Hao ni matapeli, kama wana hela za chapchap hivyoo ni bora wazipeleke m'nyamala hosptl kwenye wodi zisizo na vitanda wagonjwa wapumzike vizuri. Au la wakawape watoto wa wajomba na mashangazi zao.
Kwa taarifa yako sasa wewe ulietuma tangazo hili:
Watanzania wengi wamekuwa wakiandika sensitive info zao katika email, n.k na wengi wao hutumia birth dates zao kama password, sasa kwa kujua email addr yake na tarehe yake ya kuzaliwa, kwa mjanja wa computer ni rahisi kupata password na kuweza ku'sneak' in some one's email.
Wana JF hizi ni zama za uwazi na ujanja mwingi, so kuweni macho na matangazo kama hayo. Kwa kampuni yoyote ile iliyo makini haiwezi kutumia gmail account, watajitangazaje sasa???
Isitoshe gharama ya kumiliki jina la kikoi (domain name) la kampuni kwa mwaka haizidi hata 200000/= sasa wewe utatoaje six digit kama salary kwa mfanyakazi wako halafu ushindwe kuwa na domain name? Acha upuuzi.
Huu ni mwaka wa kurekebishana tu mpaka tuwe kama USA, UK na kwingineko......