Ana Diploma, Anapenda Kuendelea na Elimu ya Juu, Afanyeje?

MahinaVeterani

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
710
Reaction score
256
Wanajamvi,
Kuna huyu mdau. Alihitimu Kidato cha Nne miaka kadhaa iliyopita. Matokeo yake yalikuwa mabovu kwa maana ya Credits 3, D chache na Fails kadhaa. Alijiendeleza na kuhitimu Certificate na Diploma za Community Development kutoka CDTI ya Serikali. Mwaka huu hakuweza kudahiliwa katika Chuo chochote kwa sababu hana Credits 4 za Kidato cha Nne kama inavyotakiwa na TCU. Ana hamu kubwa ya kujiendeleza kwa Elimu ya Chuo Kikuu hasa kwenye Taaluma ya Community Development au Socialogy haijalishi hata kama ni kujilipia. Yuko kijijini. Anaomba msaada, kwa wenye uelewa, atumie approach ipi ili atimize ndoto yake ya kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu! Thanks in advance
 
Mmi binafsi nimemaliza diploma ya business mwaka huu. Na hvi sasa na subiri majibu ya selection toka tcu. Kwa kwel kwa mchango wangu wa kwanza tembelea home page ya tcu kuna maelezo pale. Mbili kwa uelewa wangu tcu inasumbua ya mtu toka form four kwenda juu via diploma form six wana pewa priority namba moja. Please naomba ni check 0715294119 nikueleweshe kidgo nashindwa andika vizuri maelezo yote
 
Molembe, the Suppoter, asanteni kwa support yenu wakuu - this means a lot! God bless you!

the Supporter, kama hutajali, Mdau atakipigia kesho mchana.

Usiku mwema!
 
Mkuu Ngajimala! Asante sana. Nimewasiliana tena na Mhusika Mdau usiku huu. Kesho atasafiri kutoka Kijijini Majimoto, Wilaya ya Serengeti kwenda mjini Musoma ili ajaribu kama ulivyoshauri na vilivile kumpigia "the Supporter" kama nilivyoomba kabla.
Endapo atakwama kwa lolote, ninaomba ruhusa yako nikurudie tena kupitia hapa jamvini kwa msaada zaidi! Cheers!
 
Wakuu Molembe, the Supporter na Ngajimala, mko poa? Vipi maendeleo ya maombi yenu ya Chuo? Kuna mafanikio?
 

Utaratibu upo hivi, anatakiwa awe na 4D'S kwa form four,hawaangalii C ka unavyodai. pia diploma awe na GPA ya kuanzia 2.7 na kuendelea.
 
Utaratibu upo hivi, anatakiwa awe na 4D'S kwa form four,hawaangalii C ka unavyodai. pia diploma awe na GPA ya kuanzia 2.7 na kuendelea.

Samahani hiv,izi sifa walizo weka tcu na nacte zinafanya kazi??mf;mtu mwenye GPA 3.1 anawastani wa C,but vyuo vingi vinahitaji wastani wa B,au first na second class,sasa ukisema GPA 2.7,mm sijui kama kuna mtu amepata chuo kwa hizo GPA,na je kwa mtu ambae ajapata chuo ata kimoja katika selection zake zote na ana izo sifa za TCU kuna uewezekano akatafutiwa chuo kingine na TCU??
 

Binafsi nina imani lzma upate chuo.kama uliomba kupitia NACTE na ukakuta jina lako ktk orodha ya watu waliokosa haumo ina maana umekuwa selected tayari. mm zaidi naangalia revised guidebook inavosema uwe na D-4 form 4 na diploma GPA ya kuanzia 2.7 ndo sifa mama.
 
Molembe, the Suppoter, asanteni kwa support yenu wakuu - this means a lot! God bless you!

the Supporter, kama hutajali, Mdau atakipigia kesho mchana.

Usiku mwema!

mzaz nimekusoma japokuwa umekosea maelezo, huyo jamaa ana pass tatu, cyo credit tatu, ni kwel hawez kupata digrii akiwa na pass tatu za o'level, cha msing kama yupo seriouz arud akatafute d moja ili ziwe nne, na ata hyo diploma yake magumash kwan aliimgiaje certificate akiwa na pass 3 badala ya 4?
 

Wakuu, Mdau (ni She, btw), amenijulisha kuwa leo system ya TCU imemkubali na amechagua BASO na Community Development. Ameniomba niwashukuru sana, alikuwa tayari keshakata tamaa, hasa ikizingatiwa kuwa yuko "swekeni - interior".
Mkuu Jaywacanza, huenda nilikosea kwenye maelezo yangu, ndio. Nadhani sikuelewa vizuri mwongozo ule wa TCU wa mwanzo. Nilielewa kuwa CREDITS 4 ni C 4. Kwa uelewa wangu D ni PASS na A, B na C ni CREDITS.
Kuhusu kutopata au kutopata Digrii, nadhani ni yeye na Mungu wake endapo TCU watamchagua.
Nimeshauri Plan B kama hatachaguliwa ya kufukuzia RPL kwa mwakani. Kurudia Mitihani ya Form IV ni ishu pevu!
Kuhusu umagumashi wa yeye kuingia Certificate kwa C tatu za Form IV siwezi kuliongelea. Ni miaka 4 iliyopita. Huenda taratibu ziliruhusu siku hizo. Lakini kumbuka Vyuo kama SAUT, Mzumbe na vingine wanapokea Form IV wa design hiyo kwa Certf - Dipl - Digrii 1 - PGD - Masters!
Asanteni wakuu!!
 
nadhani ni kweli utaratibu unabadilika,kuna tangazo nacte wamelitoa ambalo kama nimelielewa vema inaonyesha kuwa wanafunzi wote wa diploma ukiwaondoa waliopo vyuoni kwa sasa,hawataweza kujiunga na digrii kama hawajapata angalau E moja ya a-level
 
nadhani ni kweli utaratibu unabadilika,kuna tangazo nacte wamelitoa ambalo kama nimelielewa vema inaonyesha kuwa wanafunzi wote wa diploma ukiwaondoa waliopo vyuoni kwa sasa,hawataweza kujiunga na digrii kama hawajapata angalau E moja ya a-level

Anywayz, ngoja tuone hii episode itaishaje. Ingawa there is a lot to be done to streamline the whole process! Thanks
 

Umenikumbusha maeneo ya Majimoto hasa pale kwenye chemchem ya majimoto na kile kitongoji cha mzee Letelanga

Back to the point, wakisumbua sana si vibaya kama akaenda for Advanced Diploma ila akomae apate GPA ya kueleweka kwani ataruhusiwa kuchua masters kwani huwa inachukuliwa kama equivalent qualification though kuna baadhi ya vyuo kama UDSM lazi,a apige miezi 9 ya post graduate diploma then masters kuliko kupoteza kuomba kila siku alafu unatoswa kwani hawa TCU walitakiwa waachie vyuo vifanye selection na wao kusimamia ubora wa elimu lakini wao process kibao bila kutumia logic maana mtu upo Shinyanga unapelekwa chuo Mtwara wakati kozi unayoitaka inapatikana miji ya jirani ambako mazingira unayamudu na ukata huu wa kupanga
 
nadhani ni kweli utaratibu unabadilika,kuna tangazo nacte wamelitoa ambalo kama nimelielewa vema inaonyesha kuwa wanafunzi wote wa diploma ukiwaondoa waliopo vyuoni kwa sasa,hawataweza kujiunga na digrii kama hawajapata angalau E moja ya a-level

Ili kuboresha kwa siku za usoni isilete usumbufu kuna haja ya NACTE na TCU wakae ili mtu anapoingia Diploma aweze kuwa na initial qualification ili akitaka kujiendeleza zaidi isilete shida kama hivi mtu ana Diploma alafu tena kujiunga chuo inakuwa kasheshe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…