Ana mimba na Condom imetumika kwa usahihi

Wewe unawakia mema kweli maana hapo ujue ndoa zote mbili ziko matatani na kusababisha ongezeko la watoto mitaani. Wamalizie hiyo dhambi ya mwishoa thena watubu.

Hata we Dena jamani!
 
Mkuu,mtoa mada naomba nichepuke kidogo nje ya mada hii
Kwa upande wangu nitazungumza na wale ambao hili janga bado halijatukuta,
hapa kuna vitu viwili vya kujifunza,
1:Mke wa mtu ni sumu.
2:Msichana anapokukataa kwa muda mrefu usilazimishe na tafuta mwingine.

Nasema hivyo kwa kuwa kama mwanamama huyo asingekuwa mke wa mtu basi jamaa asingekuwa na wasiwasi na hali hiyo angelea mtoto wake tu hata kama ni wa kusingiziwa.Na hilo la pili inawezekana kuwa mwanamke ameamua kumkomesha jamaa kwa kumuona king`ang`anizi.Mwanaume unakataliwa miaka kumi bado tu hukati tamaa?Ina maana mwanamke ni huyohuyo?Huogopi wake za watu?
Hii inanikumbusha jamaa yangu mmoja aliwahi kumfuatilia msichana tangu wako form II mpaka wanamaliza form VI,na bado hakumpata,baada ya majibu jamaa yangu akafaulu vizuri na akapata nafasi ya chuo USA.Yule msichana alivyosikia alikuwa wa kwanza kujipendekeza kwa jamaa yangu na kumuonesha kuwa anampenda ajabu,ila alikuwa anampima tu ili ajue kama ana upendo wa kweli.Jamaa yangu naye kuona kakubaliwa alishukuru na ahadi nyingi zikatolewa,na kweli tendo lilitendeka mara mbili kwa kutumia kinga na jamaa akapaa zake USA.Mwezi mmoja baada ya kufika US akapokea ujumbe kuwa binti ni mjamzito,akachanganyikiwa na kujiuliza inakuwaje wakati nilitumia zana?Lakini kwa kuwa alimpenda binti akakubali shingo upande na akatoa malezi yote ya ujauzito,siku ya kujifungua bahati mbaya mwanamke akafariki akiwa leba ila mtoto akapona,ikabidi jukumu la malezi liende kwa mama mzazi wa bwana.Miaka mitano baadaye jamaa yangu akawa tayari amepata uraia wa US,na akaamua amchukue mtoto wake akaishi naye.Siku alipokwenda na mtoto ubalozini kumchukulia visa ubalozi wakasema inabidi tuchukue DNA test kuhakikisha kama mtoto ni wako kweli isijekuwa unafanya child smugling.Jamaa akakubali na majibu yalipotoka wakamwambia mtoto si wako hatutaweza kukupatia visa yake.
Sasa basi kwa hali kama hiyo jamaa inabidi awe makini sana na asikubali tu na kama atasubiri mpaka mtoto kuzaliwa inabidi kuwe na DNA test maana inaonekana hapo kuna harufu ya kukomoana,kwani nani ana uhakika kuwa hiyo mimba siyo ya huyo mume wa huyo dada?Kuna mtu yoyote ambaye huwa anawachunga wanapokuwa chumbani ambaye anaweza kuihakikishia jamii kuwa kweli hiyo mimba siyo ya mumewe?I m very sorry for my long post.
 
kipi bora watoto wa pande zote mbili wateseke au kuvunja amri ya kuua kama walivyovunja amri ya sita??? Tusaidiane hapo dear
Jamani habari ya kuua mimi sishauri kabisa, hata kama waliishafanya dhambi ya uzinzi, Mimi kuna rafiki yangui wa karibu sana alifariki baada ya kupewa dawa ambazo aliamini zingemsaidia yeye kupata ujauzito baada ya kukaa kwenye ndoa bila kupata mtoto.
Kama wengine wanakufa sababu ya kuwatafuta, PLEASE mshauri asiitoe hiyo mimba, inavyoonekana huyo dada anaafanya kazi, hata akliachwa na mume hatashindwa kulea watoto wake!
 

I m in love with............
WILL YOU MARRY ME PLEASE


PM hili swali uliulizwa mbona hujajibu lakini?? Mie narudi are you in love with who?? Maana wewe jana ulinikalia kooni mpaka nikajibu swali lako namie leo nakuuliza naomba majibu tafadhali usiniangushe
 



Nimeshamweleza ni yeye tu ndio hajajibu kitu,nimemwambia swali hili halina mwenyewe hivyo anaweza kulijibu tu akiona ana jibu zuri.
 
hivi hivyo vipimo vya DNA huwa havikosei??...
 
duh!
Hapa kuna mambo mengi unatakiwa kujua kuhusu huu msala,inawezekana story hii haipo kama walivyokwambia,inawezekana mara ya kwanza au ya pili kukutana hawakutumia kinga kwa ufasaha.pili,mwanamke anaweza kuwa anawaonea huruma watu wengine ambao wamewahi kumtongoza bila kukatatamaa.mwisho ni kifutio walichotumia,ambacho kwa mtanzania wa kawaida kuamini hili ndio source ya mimba ni ngumu.
Solution
-wakubaliane na ukweli na kuwajulisha wapenzi wao madhambi yao.
-waitoe na kila mmoja arudi kwenye ndoa yake (ingawa kwa maelezo ni kwamba hao macheater wanapendana kuzidi wanavyopenda ndoa zao)
 

Huyo jamaa ni mshari sana na kwa watu wanaomfahamu ni mtu asiyeshaurika hata na baadhi ya ndugu zake akiwemo hata baba yake mzazi na suala la kumwambia litafumua kila kitu na siyo mtu wa kuzoeleka kirahisi na hata utamzoea itamchukua muda kuweza kumweleza jambo kama hilo na huku mimba itakuwa inaendelea kukua hii imekaa vibaya kuliko ninavyoeleza.
 

Black Cat hujakosea na wala hujatoka kiwango hicho unachodhani kwa uelewa wangu ni kuwa humu jamvini ni shule tosha kwa wanaopenda kujifunza na imenifanya nitafute kufuli la zipu yangu kabisa najifunza pia kama wewe na sio kwa mke wa mtu tu bali MAHUSIANO YOYOTE YASIYO RASMI YANA MADHARA MAKUBWA NA HATA MAJUTO na kwa mke wa mtu ni balaa la zaidi na hii mada ya kwako nadhani imeleta changamoto nyingine ambayo hebu fikiria mama kafa na umelea mtoto siku zote halafu hata hujui baba yake ni nani baada ya kuambiwa siyo wa kwako unaathirika kisaikolojia.

Binafsi nashukuru sana kwa Mchango wako.
 

Mmh! hapo sasa makubwa! inabidi tu huyo dada akubali matokeo!
 
wanakudanganya akuna cha usahihi sio darasani

KUNA KONDOM ZA MWANZO ZILIKUWA ZINATOA MANANII MWANAUME AKIIMALIZA LAKINI ILIKUWA NGUMU KUYAONA NA KUPATA MIMBA AIITAJI ZOTE YAANO HATA TONE LIKIFIKA KUNAKO DIDY ANAZALIWA
MAMA YANGU MZAZI ALIZALIWA NA KONDOM NA AKIKUPA STORY ALIPOMALIZA MASOMO YAKE YA NURSE NDIO BABAKE AKAMUULIZA UNAJUA KWA NINI NAKUPENDA SANA MWANANGU..AKAMWAMBIA UNAJUA WAKATI ULIPOPATIKANA NILITUMIA KONDOM ILA NAZANI ILITOBOKA KWA MBELE..UKWELI HALISI NDIO HUO MAMA NGU AKAZALIWA NA LEO ANA WAJUKUU SO KONDOM ZIPO KAMA ZIPO ILA UKIZIDADIS SANA AZIZUII MIMBA WALA CHOCHOTE TENA ZIKITUMIKA VIZURI NA ILE MIKELELE YA MBA MBA MBA WEEEEEE LAZIMA TWINS WATOKE WALIKO
 

Nashukuru kaka huo wote ni uzoefu wa kutosha na darasa la bure
 

Kinachonipa shida zaidi ni kuwa hawa watu wanapendana sna na kuaminiana kuliko mtu mwingine anavyoweza kuwaingilia na ushauri wowote ambao nitautoa unaweza kumpendeza moja na kumuudhi mwingine nahitaji msaada wandugu
 

Mh mimi nataka kujua kwanza hii ya kwako, baada ya DNA Kuonyesha mtoto si wa jamaa ilikuaje mama wamshikaji aliendelea kumle mjukuu au walifanyaje, na huyo mtoto anamwita jamaa baba au walimwambia sio babaake, au wamemficha mpaka leo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…