Vitalis Msungwite
JF-Expert Member
- May 11, 2014
- 3,292
- 7,867
Kila karne, hususan katika kilele cha kipindi kinchoishia '20' dunia inakumbwa na maradhi makubwa ya kufisha? Yaani namaanisha: 1120, 1220, 1320, 1420, 1520, 1620, 1720, 1820, 1920, 2020, 2120.
Mwaka 1520 kiliibuka kile kile kilichoitwa Mexican Smallpox, Robert Rotberg katika ukurasa wa 107 wa kitabu chake, Population History and the Family: A Journal of Interdisciplinary History Reader. [kwa kudadavua] anaandika hivi:
"...mwaka 1519 Mexico ilikadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 25. Mwaka 1520 walikumbwa na ugonjwa wa ndui na theluthi moja walikufa kwa ugonjwa huo."
Ukaja mwaka 1620 ambao kulikuwa na maradhi yaliyoitwa Great Pestilence. Haya yaliwaathiri sana Wahindi na halaiki ya watu iliuawa.
Karne moja baadaye, yaani mwaka 1720 kikaja kile kile kilichoitwaGreat Plague (Tauni Kuu). Ilianzia katika mji wa Marseille nchini Ufaransa. Kwa muda mfupi tu iliua zaidi ya watu 100,000. Wale 50,000 walikufa katika mji huo na zaidi ya 50,000 walikufa katika maeneo mengine yanayouzingira mji huo. Haikusambaa kama corona kwa sababu usafiri nyakati hizo haukuwa mrahisi kama ilivyo sasa.
Hata hivyo, mwandishi Warren Candler Scoville katika uk. wa 169 wa kitabu chake, The Persecution of Huguenots and French Economic Development, 1680-1720', ameandika hivi: Hakuna ajuaye ni Wafaransa wangapi waliangamia. Idadi kamili haitajulikana kamwe. Wengine waliita 'bubonic plague'.
Kisha karne nyingine baadaye, yaani mwaka 1820, dunia ikakumbwa na kile kilichoitwa Cholera Outbreak (Mlipuko wa Kipindupindu). Huu ndio mwaka ambao maradhi ya kipindupindu yalijulikana kwa mara ya kwanza. Ilianza kidogo kidogo Septemba 1817 nchini India kiasi kwamba Wazungu waliuita ni Asiatic Cholera kisha ukasambaa maeneo mengi ya dunia. Maelfu ya watu walikufa.
Mwaka 1920 ukaja ugonjwa ulioitwa Mafua ya Hispania ambayo mwandishi mmoja wa Marekani, John Barry, akayaita Great Influenza katika kitabu chake, The Great Influenza: The Epic Story of the Deadliest Plague in History.' Zaidi ya watu 50,000,000 (yaani milioni 50) walikufa kutokana na mafua hayo. Mwandishi John Barry anaandika hivi: "An account of the deadly influenza epidemic ... took the lives of millions of people around the world."
Sasa umekuja mwaka 2020. Imekuja Coronavirus. Hii nayo itapita? Sijui. Najaribu kusoma historia na kujifunza.
Sent using Jamii Forums mobile app