kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Mwl wangu wa shule ya msingi alinichapia hadithi ya fisi, mfupa na jiwe. Alisema, siku moja fisi mwenye njaa Kali alikiona kitu cheupe mbali kabisa akidhani kuwa ulikuwa ni mfupa unaofaa kula na kuponya njaa yake kali. Pamoja na njaa yake alikimbia umbali mrefu kuufuata "mfupa" aliouona kwa mbali. Baada ya kufika eneo la tukio aligundua kuwa haujuwa mfupa bali jiwe jeupe, hata hivyo hakuamini kama ule haujuwa mfupa, hivyo akaupiga jino ili kuhakikisha hadi akapoteza jino lake moja. Kwa hasira fisi aliligeukia na kulijambia na kusema na wewe harufu ya ushuzi wangu umeipata, kisha huyooo akaondoka na njaa yake kwa taabu sana.
Fei Toto sasa baada ya kushindwa kufanikisha dili lake ameamua kuzungumza na kutupa lawama kwa eng. Hersi kama mtu mbaya sana na aliyesababisha aondoke siku moja kabla Ya mechi ya Yanga vs Azam fc kama vile alikuwa na mpango wa kuisaidiia Azam ishinde mechi ile.
Kufanya hivi ni sawa na kulijambia jiwe ili linuke harufu ya ushuzi angalau, maana baada ya Fei Toto kuondoka Yanga imetwaa ubingwa, imeingia fainali ya kombe la Azam cup na kucheza finali za CAF na kuhama timu hahami hadi mkataba wake uishe.