Anachokifanya Msigwa kwenye mjadala kaniongezea wasiwasi mara 100 zaidi ya niliokuwa nao

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Msigwa anaonekana kabisa kaandaa mjadala huu wa Bandari kimkakati, yupo kipropaganda, hataki kukosolewa anataka watu waongee anachotaka.

Haruhusu maswali yanayomchallenge na yakiulizwa anayajibu kisiasa anaingia anatoka kama mchwa kwenye kichuguu mwisho hujui hata kajibj nini, kifupi hana anachofanya zaidi ya kuongeza wasiwasi japo yeye anahisi anawapumbaza watu waone mkataba wa bandari uko sawa kumbe anazidisha hofu.
 
Hebu tuwekee link ili nasi tuone,kabla ya kuanza kumtukana.
 
Wasi wasi ni mkubwa zaidi..., na tena...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Hiyo namba Tatu daaah...INA MAANA NDIO TAYARI TUSHAUZWA[emoji27]
 
Wizara ya Mambo ya Nje ya Australia inaitambua Nchi ya United Arab Emirates ambayo ndani yake yapo majimbo saba : Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ajman, Umm Al-Quwain na Fujairah huku jimbo la saba la Ras Al Khaimah ilijiunga na Shirikisho la UAE mwaka 1972. Huku mji mkuu wa nchi ya UAE ikiwa ni Abu Dhabi, mji uliopo ndani ya jimbo / emirate kubwa na tajiri zaidi ya nchi ya UAE .

Rais wa shirikisho la nchi ya UAE ni maulana sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan. Kiongozi wa jimbo la Dubai maulana sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum ni Makamu wa Rais pia ni Waziri Mkuu na Waziri wa nchi ya UAE

Mahusiano baina ya Australia na nchi ya UAE ni ya kirafiki, katika nyanja mbalimbali huku yakiendelea kukua.

Nchi ya UAE ushirikiano wake na Australia umewezesha nchi hiyo ya Australia kuwa ni mwekezaji mkubwa zaidi wa mitaji na biashara nchini UAE kuliko nchi yoyote ya Masharik ya Kati.
 
Msigwa anaonekana kabisa kaandaa mjadala huu wa Bandari kimkakati, yupo kipropaganda, hataki kukosolewa anataka watu waongee anachotaka.

Haruhusu maswali yanayomchallenge na yakiulizwa anayajibu kisiasa anaingia anatoka kama mchwa kwenye kichuguu mwisho hujui hata kajibj nini, kifupi hana anachofanya zaidi ya kuongeza wasiwasi japo yeye anahisi anawapumbaza watu waone mkataba wa bandari uko sawa kumbe anazidisha hofu.
Akisoma hii atajiongeza
61f306d20d9ca1c0227f3b5820dab622.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasi wasi ni mkubwa zaidi..., na tena...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Naomba Mungu usiku na mchana waTanganyika wakawa na wivu na nchi yao. Badala ya kuwa sandakalawe.

Maswali yako ni mazuri na yenye lojiki. Swali no. 3, 5 na 6. Yangepaziwa sauti. Ujinga huu ungekoma . Wananchi waTanganyika waionee wivu nchi yao. Maandamano makubwa yangetosha kumaliza Ujinga huu.
 
Msigwa anaonekana kabisa kaandaa mjadala huu wa Bandari kimkakati, yupo kipropaganda, hataki kukosolewa anataka watu waongee anachotaka.

Haruhusu maswali yanayomchallenge na yakiulizwa anayajibu kisiasa anaingia anatoka kama mchwa kwenye kichuguu mwisho hujui hata kajibj nini, kifupi hana anachofanya zaidi ya kuongeza wasiwasi japo yeye anahisi anawapumbaza watu waone mkataba wa bandari uko sawa kumbe anazidisha hofu.
Heri yangu niliacha kuwasikiliza hawa Jamaa
 
Kwa sababu ya TUMBO basi msigwa ameamua kuuvaa ujinga na kuwa msaliti wa taifa lake na watu wake...na kwa ujinga huo huo bado anaamini anao uwezo wa kuwahadaa watanzania waumgane nae kushangilia uuzwaji wa nchi yao kwa wakoloni wa kileo...
 
Msigwa anaonekana kabisa kaandaa mjadala huu wa Bandari kimkakati, yupo kipropaganda, hataki kukosolewa anataka watu waongee anachotaka.

Haruhusu maswali yanayomchallenge na yakiulizwa anayajibu kisiasa anaingia anatoka kama mchwa kwenye kichuguu mwisho hujui hata kajibj nini, kifupi hana anachofanya zaidi ya kuongeza wasiwasi japo yeye anahisi anawapumbaza watu waone mkataba wa bandari uko sawa kumbe anazidisha hofu.
Tuna Tanzania na hatuna Tanganyika!.Mtanzania anayo haki ya kuhoji na kujibiwa,lakini kwa mizimu ya marehemu Tanganyika,haki hiyo haipo.
 
Kuna moja kablokiwa kisa kasema watanganyika hawakuhusika kwenye kusaini mkataba
Sasa huyo sinimwehu moja kwa moja!.Watu tunaijadili Tanzania,yeye anamleta marehemu Tanganyika alizikwa mwaka 1964!.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Msigwa anaonekana kabisa kaandaa mjadala huu wa Bandari kimkakati, yupo kipropaganda, hataki kukosolewa anataka watu waongee anachotaka.

Haruhusu maswali yanayomchallenge na yakiulizwa anayajibu kisiasa anaingia anatoka kama mchwa kwenye kichuguu mwisho hujui hata kajibj nini, kifupi hana anachofanya zaidi ya kuongeza wasiwasi japo yeye anahisi anawapumbaza watu waone mkataba wa bandari uko sawa kumbe anazidisha hofu.
Danganya ambao awajashiriki mm nimeshiriki watu walipewa fursa sema Kuna wajinga wawili mmoja alianza kulia na mwingine kuleta ubaguzi
 
Back
Top Bottom