sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Makosa tajiri mkubwa Iringa miaka hiyo akafirisika vibaya na kuwa mnywa visungura na mtogwa analewa 24 seven. Simulizi yake ukifika Iringa utaipata vizuri zaidi maana hakosekani maeneo ya starehe.
Diamond Platnumz ameona simulizi yake mtandaon, imemgusa na ameamua kumshika mkono.
Hivyo Diamond ameomba yoyote mwenye contact za Makosa amfikishie salamu ili atoe sadaka yake.
Ili ni funzo kwetu tunatakiwa kupunguziana maumivu, binadamu sisi hatuna ujanja kabisa kwenye maisha yetu hivyo ukiona mtu kakwama badala ya kumfanyia judgement angalia namna ya kumpiga tafu.
Kidonda hata kama ni kikubwa na kinauma akipatikana hata mtu wa kukipuliza upate dakika chache za unafuu ni jambo jema sana.
Asante sana Diamond kwa kutukumbusha ubinadamu mimi hapa jf nimekuwa balozi mzuri sana wa upendo na ubinadamu.