Anaehusika na kuset kodi za magari used TRA aangalie vizuri ushuru wa Nissan Leaf 2019 EV nataka ivuta Februari!

Kuna gari kia grand carnival sijui kwa nini hua ushuru wake ni pasua kichwa, tra wabadilike bei ya gari iko chini ila ushuru wa tra ni balaa
Wanakua hawaja update ile CIF ya sokoni. Unakuta sahivi gari used sokoni wastani ni $6,000 wao wameweka $18,000 Kwahiyo inapelekea kodi zote ziwe juu maana hesabu zao zote zinatoka % ya CIF.
 
TRA hawahusiki,wao wanatekeleza tu Sheria zilizotungwa na bunge la ndiyoooo.vigezo vya kuwa mbunge viangaliwe upya.Mbunge anatakiwa awe na uwezo wa kuchanganua mambo kuendana na wakati siyo tu kujua kusoma na kuandika kama ilivyo sasa
 
MKUU,SAMAHANI,MIMI BINAFSI SINA GARI.

ILA NATAKA KUTAVUTA HII CHUMA,NAOMBA KUJUA GHARAMA ZA ZOTE ZA KUNUNUA HADI KUFIKISHA BONGO NA USHURU WOTE WA TRA NI JUMLA HIZI 23.2M AU ZINAZIDI?

KAMA ZINAZIDI NAOMBA NISAIDIE BEI KAMILI HADI KUMILIKI.
 
Wanakua hawaja update ile CIF ya sokoni. Unakuta sahivi gari used sokoni wastani ni $6,000 wao wameweka $18,000 Kwahiyo inapelekea kodi zote ziwe juu maana hesabu zao zote zinatoka % ya CIF.
Naomba uni-refer kwenye ule uzi wako ulioelezea kuhusu miundombinu ya kuchajia EVs.
 
MKUU,SAMAHANI,MIMI BINAFSI SINA GARI.

ILA NATAKA KUTAVUTA HII CHUMA,NAOMBA KUJUA GHARAMA ZA ZOTE ZA KUNUNUA HADI KUFIKISHA BONGO NA USHURU WOTE WA TRA NI JUMLA HIZI 23.2M AU ZINAZIDI?

KAMA ZINAZIDI NAOMBA NISAIDIE BEI KAMILI HADI KUMILIKI.
Mkuu, unataka gari ya umeme Nissan Leaf 2nd generation (ZAA-ZE1)?

Mi nilikua naitaka Feb hii niivute ila nineshindwa. Kwasababu TRA wamekaza kushusha kodi.

Bei ya gari yenyewe kule JP cheap kabisa 5,500 $ ambazo ni kama Mil 14 na ushuru wake Mil 20 kwahiyo jumla kama mik 34 kwenda juu.

Kusema kweli siwezi nunua gari Mil 14 nikampa TRA mil 20. Never.
 
Naomba uni-refer kwenye ule uzi wako ulioelezea kuhusu miundombinu ya kuchajia EVs.
Wakati nautafuta, kumbuka kuchaji kuko kwa aina tatu (au niseme chaja zipo za aina tatu):

Level I: Huu ni umeme (AC current) wa nyumbani, yaani unaotumia friji, tv, pasi unachofanya utarefusha tu cable ili ifike nje uchaji gari lako. Unakua na 110-120v sema unachaji slow. Unakuta 7-8 km kwa saa 1.

Level II: Huu pia ni wa nyumbani na commercial buildings au viwandani. Pia ni AC current. Unakua na 220-240v. Huu una speed zaidi ya kuchaji kuliko Level I unaweza ingiza kilometa 20-30 kwa saa moja.

Level III: Huu ni DC current. Ni fast charger. Zipo kwenye commercial buildings au charging stations. Huu unaweza chaji ata 0-80% ndani ya Dakika 10 tu, au 20km kwa dakika.
 
HAPA,NIMESHINDWA.
 
Kwahiyo hapo kwenye level II, unatakiwa uvute umeme kutokea wapi hadi nyumbani?.
 
Kwahiyo hapo kwenye level II, unatakiwa uvute umeme kutokea wapi hadi nyumbani?.
Hapo itabidi uongee na fundi umeme wako, au TANESCO ili uwe na huo 240V nyumbani kwako. Sijui ndio three phase wanaita. Kwa matumizi ya kawaida, let say kwenda na kurudi kazini chini ya kilometa 100 kwa siku, Level I inatosha.

Level II kama unataka kujaza full charge let's say 0-100% ndani ya usiku mmoja (7pm hadi 7am), kitu ambacho sio kizuri kumaliza 0% ya battery (iwe ni gari, simu nk) na pia sio kizuri kujaza hadi 100%.
 
single phase 240 V
three phase 400 V
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…