Anaejua mambo ya leseni za salon ndogo

Anaejua mambo ya leseni za salon ndogo

MOONFISH

Senior Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
135
Reaction score
268
Habari wajuba hope mko poa sana.

Kuna thread nilileta huku japo wachangiaji walikuwa ni wachache ila nilifanikiwa kumfungulia dogo salon ni ndogo na ya kawaida sasa swali langu nilikuwa ni kujua kama kuna huitaji wa leseni maana saloon nimefungulia nje ya mji na gharama zake zilienda kama laki saba.

Ningependa mtu mwenye utaalamu na haya mambo nijue maana nisije nikavamiwa siku na TRA ikawa tena kisanga kwangu.

Natanguliza shukrani kwa wote watakao nipa ushauri na mapovu ruksa. hallaa!!!!
 
Nenda halmashauri chumba cha biashara waambie unataka leseni mpya, kuna Fomu utajaza pale, Utaenda TRA kufanya Clearance, unapigwa hela kutokana na unavoenda kufanyiwa makadilio, Saluni ndogo unaweza lipia 25,000 mpaka 60,000 TRA.

Ukimaliza apo unapita kwa Mtendaji wa kata ama Mwenyekiti kugongewa muhuli, Then unaenda halmashauri sasa kupigwa za uso, [emoji28] Hapo wanakukadilia Sasa unaweza lipia Laki, ama laki na nusu
 
-mbona kama gharama zina ongezeka sasa si bora nikae kimya
 
Kwa usalama nenda kwenye mamlaka husika.
Au piga kimya ukiona waaleeee unafunga kwa muda mpaka wapite.
 
wewe nenda halmashauri kachukue fomu ujaze lakini kwani umeshafungua jina la biashara brela na unayo tin maana kabla hujaanza leseni inabidi uwe navyo hivyo ndo uende kwenye leseni
 
Back
Top Bottom