Anaezifahamu vizuri gari aina ya Toyota Vanguard na Harrier msaada tafadhali

Cheef Baroka

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2019
Posts
491
Reaction score
1,010
Habari: Wakuu kuna "Kampuni" moja ya kigeni nimekuwa nikifanya nayo kazi kwa vipindi tofauti kila wanapopata tenda hapa Tz. Sasa kuna mradi wamemaliza na juzi wamekabidhi kwa mafanikio makubwa huku wakipew big" YES" na Wizara husika.

Sasa kuna kiasi flan cha Pesa bado nawadai but hawataki kunipa cash.

wanasema nichague waniachie gari moja kati ya hizo mbili. Sasa nimewaza nikilazimisha pesa2 ntakosa vyote mana ni muda tunasumbuana. Nimeona niombe Wataalam wa Magari mnijuze Thamani ya gari hizo, ubora, utumiaji wa mafuta na ipi nichukue kati ya hizo,?. Kwa harakaharaka Gari hizo walikuja nazo bado mpya na zimetumika miaka 2 na miezi3 na siku 17. kiasi nachowadai ni km Usd 6230. Je ni ipi nikichukua kati ya hizo gari nikiuza hata kwa bei ya hasara nitarudisha pesa yangu.

 
Kwanza hizo 14.3 Million unazodai ni kidogo sana ukilinganisha na mfumuko wa bei za magari sahivi kwa bongo. Van Guard ni kaka yake RAV4, chukua hiyo hutajutia kama ina engine ya VVTi lita moja ninakupeleka 10-14km kutegema na uchakavu wake. Achana na Harrier ni jini la kubugia mafuta
 
Hayo magari kama yaliingizwa bila kodi jiandae pia kulipia kodi,nadhani table ya kodi imewekwa hapo juu.Labda kama watakulipia kodi wenyewe,kitu ambacho najua hawawezi maana kodi itazidi hizo usd 6k unazowadai

Ila kama walishalipia kodi basi poa ,wakusaidie kubadilisha ownership maana TRA kwa sasa hawaeleweki sana wanaweza kuku charge capital gain tax,kwa kutafuta tofauti ya bei ya soko kwa hizo gari na kiasi ambacho wewe umewalipa ambacho ni hizo unazowadai.

otherwise wakuachie gari yao pamoja na docs ,wewe uendelee kutumia bila kubadili umiliki.Ila siku ukipata ajali malipo ya Bima itabidi yaingie kwenye akaunti inayosoma jina la mmiliki
 
Shukrani kaka. me siyajui sana magari ko kuna fundi nimemleta kuzikagua anasema bado nzima na hazijabadilishwa kifaa chochote cha ndani ukiacha cover za sit
 
Umenifungua akili kaka . "Why iwe rahisi kuachia gari linalozidi thamani pesa nazodai afu iwe ngum kunilipa cash?". huenda naachiwa msala kaka .

Lakini pia, Ivi inawezekana gari likaingia nchini toka 2018 mwishon lika fuction mpaka leo bila kulipiwa kodi kweli?
 
Kama lina exemption,yes inawezekana mkuu.
 
Kuna miradi inapataga misamaha ya kodi ya kuingiza vifaa vya miradi.vifaa hivyo vikuzwa anaye nunua anatakiwa kulipia ile kodi iliyosamehewa kwa thamani ya kile kitu kwa wakati kinauzwa.

Hivyo kama hayo magari yalipata msamaha wakati wa manunuzi,jua ukinunua utatakiwa kulipia kodi,kwa sababu madhumuni ya gari yanakuwa yamebadilika kutoka kuwa la mradi na kuwa la mtu binafs
 
Sina chakukulipeni Wakuu. mmenifungua vizuri sana. Ko ili nijue kama limelipiwa au lina exemption pa bila wao kujua nifanyeje? nikienda Tra na plt number wanaweza niangalizia au njia gani nitumie?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…