makaveli10
JF-Expert Member
- Mar 27, 2013
- 31,583
- 92,670
Ndugu zangu nimekwama, tena nimekwama haswa. Nimegadhibika pasina mfano 😠😡, mimi si mtu wa kwenda vilingeni ila kwa hili Mola wangu anisamehe sana.
Shambani nina minazi takribani 100 ila siambulii kitu,
Hawa waduwanzi naona sasa wanaleta mazoea yasiyovumilika. Zamani kila baada ya miezi mitatu nilikuwa navuna nazi najaza canter ya tani 4 vizuri tu. Taaratiiibu mambo yakawa yanabadilika, nazi 2000+ zikaja kuwa navuna nazi 800+, ikashuka ikawa naambulia nazi 300+, ikaja nazi 100 na hapo ni za kutafuta haswa, naangua mpaka ambazo si kavu.
Hawajatosheka sasa wanaangua mpaka madafu, nafika nakuta minazi hakuna kitu, nimevumilia nimechoka.
Hii ni tabia ambayo kijiji kile imeota pembe. Sasa basi nahitaji mtaalam ambae anaweza kumgandisha mtu shambani na zigo lake aliloiba, sitaki kuua wala kutiana uchizi, nataka nimkute mtu yupo shambani mwangu na zigo lake la nazi.
Malipo ni baada ya kazi kufanyika na matokeo chanya kupatikana.
Ninajaribu kuwatag kina mshanajr, mzizimkavu, likud na wengineo inagoma.