Anahitajika Mwalimu wa Kujitolea kufundisha Shule ya English Medium

Anahitajika Mwalimu wa Kujitolea kufundisha Shule ya English Medium

wadzelino

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2019
Posts
225
Reaction score
385
Anahitajika mwalimu wa kujitolea hasa wa kike, awe na uwezo wa kufundisha darasa I na II, hata chini ya hapo siyo mbaya. Awe mahiri wa lugha za Kiingereza na Kiswahili, hasa kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha.

Atajitolea miezi mitatu, then atapewa mkataba kamili, kipindi anajitolea atalipwa posho, atapewa sehemu ya kulala pia.

Aliye tayari anakaribishwa.
 
Anahitajika mwalimu wa kujitolea hasa wa kike,awe na uwezo wa kufundisha darasa I na II,hata chini ya hapo siyo mbaya.
Awe mahiri wa lugha za Kiingereza na kiswahili,hasa kuzungumza kiingereza kwa ufasaha.

Atajitolea miezi mitatu,then atapewa mkataba kamili,kipindi anajitolea atalipwa posho,atapewa sehemu ya kulala pia.

Aliye tayari anakaribishwa.
Una shule au kituo cha daycare?
 
Anahitajika mwalimu wa kujitolea hasa wa kike, awe na uwezo wa kufundisha darasa I na II, hata chini ya hapo siyo mbaya. Awe mahiri wa lugha za Kiingereza na Kiswahili, hasa kuzungumza Kiingereza kwa ufasaha.

Atajitolea miezi mitatu, then atapewa mkataba kamili, kipindi anajitolea atalipwa posho, atapewa sehemu ya kulala pia.

Aliye tayari anakaribishwa.
Mimi hapa mkuu. Nina degree ya catering na ninaongea na kuandika kiingereza swafi.

Ngoja kwanza nimfungulie shemeji yangu geti anapiga honi halafu nitarudi kujieleza zaidi.
 
Nimependa sana hii, laiti ningekuwa jirani na ulipo ningejitolea chap....... naomba nikutafutie vijana wenye moyo wa kujitolea....!
 
Kila atakayeona huu ni utumbo ni kwavile yupo kwenye ajira na anacomment hovyo kukatisha tamaa wenzake.

Huyu mtu kabla ya kujitolea alikua anakula wapi?

Mwenye shule hajui unaweza ongeza nini kwenye shule yake huna uzoefu zaidi ya field halafu unataka aanze tu kukutreat kama mwajiriwa?

Kama teacher anaweza abargain na HM. Kiasi cha posho, kiasi cha mshahara akionekana anafaa, chance ya kutumia shule yake kama reference akiomba kazi kwingine, targets ambazo zitadetermine kama agewe mkataba ama la, na ikiwezekana baada ya mwezi ishu ya kula ijumuishwe.
 
Back
Top Bottom