Anaimba tangu 2020 kawahi kupata show mbili za laki 1 na elf 20, Nawezaje kumshawishi ajikite zaidi na vitu vingine vya kimaendeleo

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
naona anakoenda siko kabisa nami kama mtu mzima niliyeweza kujionea uhalisia wa muziki ni wasanii wachache sana wanaoweza kupenya na wengi hawafiki kokote na hata kuharibu maisha ya baadhi ya vijana ninasikitika kwamba dogo anaweza kuingia huko.

Mara kadhaa anashea nami miziki yake kwa whatsapp huwa nampa moyo na anajua kuimba tatizo uhalisia ni kwamba mziki wa Tz hadi utoboe ni mambo mengi sana.

Sina tatizo na yeye kufanya mziki maana ni kitu anachipenda na ni ngumu kuacha ila shida inapokuja ni kwamba hafanyi wala kujifunza mambo mengine ya kumuingizia kipato, anategemea muziki uje kumpa pesa.

Muziki wake maarufu zaidi una viewers / watazamani elfu 2, comments 3 ikiwemo yangu ya kumpongeza

Show alizowahi kuitwa ni mbili tu, Ya kwanza aliitwa 2021 kaifanya kwa elf 70, ya pili mwaka jana kwa elf 50
 
Dogo akomae na huo mziki kama anafanya kwa mapenzi kabisa,kuna siku atatoboa tu.
Tunaangalia na maisha mkuu, Ufanye kitu ambacho kimekuingizia shilingi laki 1 na elf 20 kwa miaka mitano ? upo serious ?

Kuna wanamuziki wengi sana hii nchi lakini hawafikii asilimia 3 walioweza kuufanya muziki uweke ugali mezani
 
Music industry ina hela

Mnunulie speaker akodishe
Mfungulie library aweke watu miziki
Mpe mtaji auze redio,flash,memory n.k
N.k na n.k
Akomae nao ila pua ajishughulishe na related business km nilivoziweka jyu na wengine waziongeze.
 
Tunaangalia na maisha mkuu, Ufanye kitu ambacho kimekuingizia shilingi laki 1 na elf 20 kwa miaka mitano ? upo serious ?
Ila ni kweli nyie kizazi cha 2000 huwa hamna uvumilivu 🀣 mwambie dogo aachane na hizo mishe atafute kazi ya kumletea pesa za haraka.
 
Mi ni mwanamuziki kama huyo dogo ila hadi sasa nina nyimbo kama mia mbili ila sijarecord popote ninaumiza kichwA nije niwe na aina yangu ya mziki huyo dogo afanye kitu tofauti na kinachosikika hivi sasa mimi kuna siku nitatoboa ila nitakuja tofauti na mziki waliozoea watu.Siku hizi watu hawatoboi kwenye shoo kuna mitandao ya kijamii ila mwambie au kama ni wewe umiza kichwa.
 
Mitandao ya kijamii inaingiza pesa lakini hadi uwe na wafuasi wengi kupata madili ya udhamini wa bidhaa, malipo ya views, n.k.

hivi kurekodi huwa ni sh ngapi,
 
Namjua huyo na comment yako nimeiona so nawe nakujua. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Music industry ina hela

Mnunulie speaker akodishe
Mfungulie library aweke watu miziki
Mpe mtaji auze redio,flash,memory n.k
N.k na n.k
Akomae nao ila pua ajishughulishe na related business km nilivoziweka jyu na wengine waziongeze.
Umeelewa lakini mtoa mada amesema dogo ni msanii sio mfanya biashara..yanibyeye anataka mambo ya hiiiyoooo... hiiiyooo..!πŸ”ŠπŸŽ€πŸŽ€πŸŽ€πŸŽ§πŸŽΆ
 
We misso misondo ,umepigaje apo
! Asee muache dgo aendelee na muziki akiwa anatafuta na ishu ingine. Kuna watu wanamaliza mwaka hawajashika ef 50 sembuse laki! Tena bora yy hiyo laki na 20 kaipata yote kwa mkupuo ,kun watu mwaka mzima jumla ya pesa yote aliyoingiza haifiki hiyo, wanaishi tu kwa kuwa kuna ndugu, jamaa na mariki wanawasapoti kwa chakula ,malazi nk.
 
Music inahitaji mtu talented sanaaaaaaaaaa..

Sasa toka 2000 mpaka leo na bado yupo yupo tuu... πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Anaimba bolingo nini
 
Mitandao ya kijamii inaingiza pesa lakini hadi uwe na wafuasi wengi kupata madili ya udhamini wa bidhaa, malipo ya views, n.k.

hivi kurekodi huwa ni sh ngapi,
Mi sijawahi kurecord ila kuna studio wanafanya hadi kwa 50000,kikubwa afanye kitu cha tofauti hapo ndo inapatikana kitu kinachoitwA mwanamuziki, yaani ni zaidi ya mashairi unayotunga.
 
kama hutajali naomba link ya channel yake youtube au kwenye platform yoyote alikopakia nyimbo zake nikamtathimini halafu nikupe mrejesho na ushauri.
 
unataka kubadilisha upepo mkuu? inawezekana ila siyo jambo rahisi hata kidogo
 
πŸ˜…πŸ˜… mwamba uko apo kwakua tu ujui kesho atakua nani .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…