Anaitwa Narrow Bee Fly sio Nairobi Fly

Anaitwa Narrow Bee Fly sio Nairobi Fly

Mtini

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
1,492
Reaction score
2,361
Wabongo wengi tumezoea kumuita Nairobi Fly, mara ya kwanza kujua kuna mdudu kama huyu ilikuwa mwaka 2005 nikiwa A level. Niliposikia wanamuita Nairobi Fly nikajua kuwa ni wadudu wenye asili ya Nairobi Kenya kumbe jina lake ni Narrow Bee Fly.

FB_IMG_1580368010196.jpg
 
Hawana huruma hata kidogo, bora hata ya nyuki kuliko hawa wadudu, kashikashi lake si lakuhadisia.
 
Wabongo wengi tumezoea kumuita Nairobi Fly, mara ya kwanza kujua kuna mdudu kama huyu ilikuwa mwaka 2005 nikiwa A level. Niliposikia wanamuita Nairobi Fly nikajua kuwa ni wadudu wenye asili ya Nairobi Kenya kumbe jina lake ni Narrow Bee FlyView attachment 1340604
Mambo ni mengi na Watanzania ni wavivu wa kujifunza.
 
Zongwe hatari sana.... Anakubabua uso hadi unakubaliwa tu na mzazi wako.
 
Nilikutana nao nikiwa a level pale longido. Ila hata leo nilikuwa najua wanaitwa nairobi fly, shukrani kwa kunifumbua macho mkuu.
 
Mkuu yote mawili ni majina ya huyo mdudu yaani Nairobi Fly au Narrow bee Fly ni sawa yote yanahusha aina mbili za beetle kisayansi wanamuita Paederus sabaeus na Paederus eximius na literature zinaonesha kuwa wanakuwa wengi Kenya wakati wa mvua nyingi. Lakini pia hujulikana kama "acid fly" au " champion fly" tazama reference hii Nairobi Fly - Wilderness & Environmental Medicine by KV Iserson - ‎2012 pia hii
Literature review of the causes, treatment, and prevention of dermatitis linearis by Brooke A. Beaulieu, Seth R. Irish
 
Huyo mdudu ukimgoogle kwa NARROW BEE FLY bado google inamleta kama NAIROBI FLY ina maana Google nao washamba kama waTz!?.
Screenshot_20200207-160757~2.jpg

Screenshot_20200207-160839~2.jpg

Au ni ushamba wa mleta mada!?..
 
Huyo mdudu ukimgoogle kwa NARROW BEE FLY bado google inamleta kama NAIROBI FLY ina maana Google nao washamba kama waTz!?.
Au ni ushamba wa mleta mada!?..

Story za vijiweni zinatuchukua sana, sasa kaambiwa huko ni Narrow bee nae akakurupuka bila kujiridhisha. Kuna mmoja nilibishana nae siku moja akaamua kuingia google akawa mpole.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Itakuwa mkenya aliamua kutafuta kiki,ila alifanikiwaa.
 
Story za vijiweni zinatuchukua sana, sasa kaambiwa huko ni Narrow bee nae akakurupuka bila kujiridhisha. Kuna mmoja nilibishana nae siku moja akaamua kuingia google akawa mpole.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Na kuna wajuaji washamba badala ya kujihakikishia wamezama kuchangia kwa kuwaponda watz wenzao!..
shame!.
 
Back
Top Bottom