Huu ndio ushauri tuliompa mwanzo kuwa amtafutie shughuli ya kufanya, lakini kama walivyosema wazazi wa binti siku ya harusi yule mwanamke hataki kufanya kazi ni mvivu sana.
Kama ameamua kuwa jeuri kiasi hicho
Mwambie huyo rafiki yako achukue likizo
asafiri kwa wiki au mbili
Asiache matumzi wala nini..
labda hapo ataitambua thamani ya mumeo..
Kweli kabisa nadhani ni inferiority complex.................hivi elimu haiwezi kuwa imechangia maana mama mwenyewe ni darasa la saba.Huyo mwanamke ana inferiority kama anaweza amtafutie hata cha kusoma awe busy, na kama ni mjeuri wa asili basi mume amtolee uvivu amuonyeshe yeye sio zoba. Na kwa kuwa bazazi banajua tabia ya binti yao basi awaeleze. Pole yake sana.
Ahahahahaaaaahhh!! Hii tulishamwambia mpaka tumechoka.
Kuna siku alimripoti kwa wazazi wake(wakwe zake) wakamwambia kama amemshindwa amrudishe kwanza kwa muda, jamaa akasita eti kwa kuwa mke wake ni mjamzito!! Kwa kweli nilimshangaa sana.Ushauri amrudishe huyo mama nyumbani kwao kwa muda wa mwaka mmoja au hata miezi sita asimpe matumizi mahitaji ya mtoto awe ananunua mwenyewe, na kwa sababu huyo mama hafanyi kazi baada ya huo muda atakua amekula jeuri yake na kujifunza. Na kama baada ya huo muda hajajifunza basi hafai ampe talaka sio ubavu wake huo atapata ugonjwa wa moyo. Ila ampe muda wa kujirekebisha kwanza asimuache moja kwa moja ghafla.
Ahahahahaaaah!! Dena mimi nina miliki baiskeli........lol...Kama ni hivyo mshauri siku moja aombe ruhusa halafu mpandishe kwenye gari yako bila kumwambia unampeleka wapi nenda nae mkoa wa jirani mnyang'anye simu zima mkalishe hapo kwa huo muda alioomba ruhusa asiwasiliane na mkewe halafu hakikisha haachi pesa ya chakula kama wengine walivyosema lazima atashika adabu tu
Kwa jinsi hali ilivyofikia hivi sasa talaka ndio suluhisho..
Ushauri amrudishe huyo mama nyumbani kwao kwa muda wa mwaka mmoja au hata miezi sita asimpe matumizi mahitaji ya mtoto awe ananunua mwenyewe, na kwa sababu huyo mama hafanyi kazi baada ya huo muda atakua amekula jeuri yake na kujifunza. Na kama baada ya huo muda hajajifunza basi hafai ampe talaka sio ubavu wake huo atapata ugonjwa wa moyo. Ila ampe muda wa kujirekebisha kwanza asimuache moja kwa moja ghafla.
Ahahahahaaaah!! Dena mimi nina miliki baiskeli........lol...
Hivi unaanzaje kumkatalia mume kutoka jamani huyu dada ni mwehu, kweli maty amrudishe tu home akanywe chai
Heshima wakuu...
Kuna jamaa yangu ambaye tumekuwa pamoja nikiwa na maana michezo ya utotoni na shule ya msingi pia tumesoma darasa moja kule kijijini kwetu. Amekuwa kama ndugu maana ndiye alinipokea hapa mjini kabla sijaanza kujitegemea. Matatizo yalianza alipooa, baada ya miezi kama sita hivi nilipigwa marufuku na mkewe nisiwe na mazoea na huyu jamaa eti namtafutia wanawake, pindi tunapotoka pamoja hasa siku za wikendi. Kuepusha mgogoro nikaacha kwenda nyumbani kwa jamaa na kama kuna shida ya muhimu namuibukia ofisini kwake. Si mimi tu, bali marafiki wote wa karibu wa jamaa walipigwa mkwara kama mimi.
Ishu ni juzi huyu jamaa kaja kuniomba ushauri amfanye nini mkewe maana kero zimezidi, akichelewa kurudi kazini ni zogo, na akirudi haruhusiwi kutoka labda atoe sababu za msingi kwa nini anatoka na ikiwezekana wanatoka wote. Kifupi jamaa hana sauti mbele ya mkewe.
Nilimshauri jamaa hii ishu aifikishe kwa wazee akianza na mshenga, kabla ya kuchukua uamuzi. Mke wa jamaa ni mama wa nyumbani.
Nimeileta hapa ili tupate uzoefu kutoka kwa wataalamu wa mahusiano na mapenzi huenda tukapata uzoefu kwa waliowahi kupata mkasa kama huu.
Nawasilisha...
Kweli kabisa nadhani ni inferiority complex.................hivi elimu haiwezi kuwa imechangia maana mama mwenyewe ni darasa la saba.
Kwa jinsi hali ilivyofikia hivi sasa talaka ndio suluhisho..