Anakatazwa kutoka ndani!!

sipati picha eti mida hii niwe nyumbani labda kama naumwa...
 
Mmmh pole sana Kaka ake Katavi.
Mwambie atumie akili za mwanaume hapo.
Usikute na yeye kashajiona hamwezi huyo mwana mama,
Asjijekuwa mume ***** bureeeeeeeee!!!!
Ajitaihidi bwana, Kuonesha yeye ni kichwa cha nyumba,
Kama vipi huyo mwanamama aamue moja kumheshimu mume wake, au akaishi kama anavyotaka.
Ye kama anajua hataki kutawaliwa kwa nini aolewe kumtesa kaka wa watu, sipati picha mkaka unakoromewa na mdada,
ndani ya nyumba.

Mmmmh nasikia Wasukuma ni wapole sana, ni kweli jamani?
Au huo jamaa atakuwa msukuma nini?
 
Duh! Mtoto mdogo sana hafai kuacha, na kwa kuwa mama hana kazi, jamaa akiondoka mtoto atateseka sana. Manake mama akikosa matunzo atamlekeza mtoto na ni mwanzo wa kuharibu msing mzima wa maisha mtoto wetu. Sasa namshauri huyu jamaa atulie mtoto akue hadi atleast 3 yrs wakuu. Wakati anavuta subira kwanza amweke mke wake chini na kumpa masharti ya kuishi hapo ndani. Ageuke tu Gaddaf kwa muda wa wk mbili. Jamaa amekua mpole mno Katavi! Si awe na kauli ya kiume, nini maana yake, hata kama ni mapenzi, hayo ya mshikaji yamekuwa kero kupita maelezo. . Inaonekana huyo jamaa ni mgumu wa kuelewa, coz mpaka Katavi unaamua kuleta hii mada humu mtakuwa mmemshauri vya kutosha. Na kama atendelea kupuuzia ushauri alopewa kote, itakuwa ameamua lolote limkute ila hamwachi mkewe, hata tumfanyeje kamwe hatobalikika. Wasiwasi wangu ni kwamba kwa maisha haya hata utendaji wake utashuka sana na unaweza kumletea madhara kazini na mwishowe kuikosa hiyo kazi. Hatuombei litokee hata kidogo, Mungu asaidie sana. Kuna mambo yakuvumilia, lakini sio hili la kuteswa na mpenzi wako uliemkabidhi moyo akaamua kuchoma na msumari, kisha ana amani wakati wewe anaumia. unaweza vumilila yote lakini sio mateso ya mapenzi. Huyo jamaa atakuwa na moyo wa plastick tofauti na wengine wenye mioyo ya nyama!
 
Tumemshauri sana aisee mwaka mmoja sasa, ushauri wako umetulia sana!
 
Ushauri wako umetulia aisee, asante
 
Ahahahaaaaahhh wakikusikia wenyewe!!! Sio wa huko ni "ndugu" wa Pinda
 
Ha ha haaaaa mkuu KATAVI embu tuambie vizuri bwana unakaufundi kidogo kwenye udalali wa wanawake?mbona mama wa watu anakuwa na wasiwasi na wewe?

kweli hiyo ni balaa huyu mwanamke ni mnafiki tu kwani jamaa wakati anamchumbia hakuwa na marafiki?kama aliwaona hao marafiki kwanini asiseme mtazamo wake wakati huo?ili jamaa achague moja mapema?Mtu mzima hafungiwii au kuchungwa hivyo tena asipoangalia atamharibu zaidi mme wake.

Minawasiwasi huyo mama yeye ndiye mwenye tabia mbaya kwanini awe na wasiwasi na mwenzake kiasi hicho?

Japo pia nimuhimu kuwa na muda na familia sio busy 24/7 lakini hilo ni suala ambalo wanandoa wanatakia kulielewa wenyewe na sio kufungiana.

Kama unataka kumkamata kuku unamwaga mtama kuku anakuja mwenyewe.Sio kupiga kwa manati!

Ushauri kwa wanawake:Ongezeni ubunifu msifungie wenzenu!!!!
 
Mwambie jamaa aongee na mkewe. Amuelezee kabisa kuwa maisha wanayoishi hayafurahii. Asipobadilika jamaa awe mkali. Asije akaanza kuchapwa viboko bure.
Kama vipi amtaftie shughuli ya kufanya huyo mkewe. Labda anachoka kukaa nyumbani ndio maana visa haviishi
 
Ahahahaah me sio dalali wala nini, na wala sikuhusika katika mchakato wowote zaidi ya harusi!
 
Sijui kama atafanya kazi yoyote maana ni mvivu balaa!
 
Katavi vipi leo jamaa bado kawekewa ngumu na wife wake isije ikawa kakatazwa hata kwenda kazini hebu cheki na mshikaji wako banaa:lol::lol:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…