Analazimisha nifanyeje?

Mnyahati

Member
Joined
Mar 5, 2012
Posts
22
Reaction score
0
kuna binti nilimtokea na alikubali kuwa mchumba wangu. Baada ya mwezi mmoja iv nilienda kumtembelea kwao na kumkuta akiwatukana wazaz wake livelive, kuanzia siku hiyo mayon mwangu nilimtoa kabisa kwan hata majirani walinidhibitishia kuwa hiyo ndo tabia yake. Mentally yuko fit na ameua six this year. Nilimwabia ukwel kuwa simhitaji tena lkn analazimisha nifanyeje?
 
kama kweli humuhitaji basi simamia uamuzi wako... sidhani kama anaweza kukulazimisha uwe naye unless na wewe mwenyewe uwe design ya 'sitaki nataka'
 
.
Kama ulikua unataka kungonoka poa, kama kuoa sahau!
 

Pole sana kaka.
Ila inaonekana ulimtamani tu,kama ungempenda hiyo sio sababu
hasa ukizingatia kuwa hauja chukua hatua yoyote kumsaidia aiache.

Kama unatafuta malaika,ume chemka maana hauta mpata.
Kama ume mpenda muite na mwambie ali kukwaza sana kwa ulicho kiona
na unapenda awe mke wako ila kwa tabia hiyo,rekebisha.
Akishindikana baada ya kuongea nae,na marafiki zake etc. hapo sawa,lakini sio unavo fanya sasa.
 

n'shamwambia lkn siku nyingine alimkemea hata kakake pia
 

hiyo sio tatizo sana mkuu, u can still have her na kila kitu kikaenda sawa... ndoa ni mkataba na kila mkataba una makubaliano yake.. jitahidi tu kwenye makubaliano yenu liwepo la kutokukutukana wewe na wazazi wako basi... hilo na kuwatukana wazazi wake ni juu yake na wazazi wake ambao walishindwa kummodify kitabia... ! akishindwa kucomply na agreements sheria ile mkondo wake.
 

Kama anakulazimisha muoe; I mean marry her, huna jinsi.
 
Kama kwa maneno haskii mwambie umeathirika na lile gonjwa letu. Hii trick niliwahi kuitumia na iliwork
 
Angalie isije ikaw kesi baadaye, huwa wanavua Condom ili wapate mimba ya lazima baadaye akwambie muoane ili kutunza mtoto pamoja

Na alivyo asha ngedere atakufata hadi ofisini akumwagie ma-nzi! Utakoma mwenyewe! We achana na huyo psycho anatukana hadi madingi zake huyo ni mwehu!
Ukila mzigo utajuta, kwanza anaacha bra, kesho anaancha chupi, keshokutwa kanga na chanuo na creme, sandals! Wiki ikiisha anakuja kufua nguo zako na kufagia na unakuta kapika misosi. Wiki ya pili na ya tatu, utamuelewa varangati yake!
 
kama unampenda kweli jitaidi kumrekebisha iyo tabia ikishindikana basi ndio umuache
 
watu tuna mapungufu lakini ya kuwatukana wazazi wako thats too much, next time atawatukana hadi wazazi wako, mwenye macho haambiwi tazama.
chukua maamuzi ingawa no one is perfect.
 
Dalili za mvua ni mawingu. Kama ameweza kuwatukana wazazi waliomleta duniani na kumsomesha mpaka kamaliza hiyo six, sidhani kama wewe pia utakuja kusalimika na hayo matusi yake.

Nafikiri umepata neema ya kujua hili tatizo mapema kabla haujajifunga na kitanzi cha ndoa. Simamia msimamo wako kukwepa matusi yatakayokuja kukupata wewe na wazazi wako baada ya ndoa ambayo yatakufanya uje uione dunia chungu.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…