AshaDii, samahani nimeshindwa ku-attach swali lako kutokana na mtandao kuwa down....... lakini nitakujibu kama ifuatavyo:
kama ni mimi Mtambuzi, kwanza kabisa, naomba ukubaliane na mimi kuwa yule ni mama yangu na atabaki kuwa mama yangu, lakini pia mke anayo nafasi yake kwangu na anazo haki zake kwangu, kwa wale wasomaji wa vitabu vya dini watakubaliana nami kuwa katika kitabu cha KIKRISTO. I mean Bible imebaishwa kwamba mtoto atawaacha wazazi wake na kwenda kuanza maisha na mkewe au mumewe, kama ilivyokuwa kwa mama na baba yako, waliwaacha wazazi wao na kuishi pamoja na kutengeneza familia, sasa iweje aniletee KIDAMISI KWENYE NDOA YANGU?
Nitakuwa muwazi, maana kama nitamuendekeza atanivurugia ndoa yangu, nitamwambia ukweli kama atakuwa na nia ya kutaka kuivuruga ndoa yangu, na kama mke wangu ndiye mwenye tatizo, itabidi nichunguze ili nijue sababu, na nikishajua sababu, bila shaka nitajua namna ya kulitatua.
Mama anayo nafasi yake kama mama na si vinginevyo........
Nadhani nimekujibu.