Ananililia niondoke nae kwenda mkoani

Cosovo

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2018
Posts
667
Reaction score
1,810
Habari zenu wanajamvi

Nilifika hapa Dar mwaka jana kwa kazi maalum kwa muda kwenye kampuni yetu

Katika harakati zangu za kijamii nilikutana na dada mmoja ambaye ametokea kunipenda sana,na kuamua kuanzisha mahusiano ya kimapenzi,na mkataba wetu ulikuwa ni mapenzi tu,bahati mbaya huyu dada ni mke wa mtu,aliolewa ila tangu aolewe mme wake aliondoka kwenda mkoani kwao kigoma miaka 2 hajarudi kumuona na hawaasiliani na bahati mbaya zaidi huyu dada ajui kwao mwanaume huko kigoma

Tangu juzi nilipomwambia naondoka Dar kurudi kazini kwangu mkoani,dada ananililia sana na kuomba niondoke nae ila ana watoto wawili,mmoja alizaa akiwa shule mwingine alizaa na mwanaume aliyemuoa

Namuonea huruma ,natamani niondoke nae ila moyo unasita kwa sababu ni mke wa mtu maana alilipiwa mahali kwa mjomba kozi wazazi wake walishatangulia

Naombeni ushauri wanajamvi
 
Daah!!! Usiondoke nae. mwambie ukweli kwamba lazima mfanye kuhakikisha kama Mme wake alishamtelekeza moja kwa moja then ndiyo mfikirie mnachofikiria ni sahihi kufanya. Aidha, mwambie kwamba mnajipa muda ili kuweka mazingira mazuri ya kuishi salama kila mmoja wenu....

Then wewe sepa....
 
Poa ndugu
 
Miaka miwili hakuna mawasiliano na mume wake bado anasema ameolewa? Mahari imetolewaje ikiwa hawafahamu wakwe zake? Wazazi wake walipokeaje mahari bila kujua ukweni. Fanya mawasiliano mazuri kabla hujafanya maamuzi ya kuondoka nae isije ikawa ni mtego.
 
Mapenzi na mahusiano hayanaga format au formula maalumu we jilipue unavyoona inafaa.
 
Kwani walifunga ndoa, kama ndio fanya uchunguzi mumewe yuko wapi na kwa nini, pengine mwenzio kakimbia vitimbwi wewe unauvaa bila kujua, ila kama, kama hawajafunga ndoa jiandae kurudisha mahari, na umuoe baada ya kumchunguza, plz usikurupuke ukafia kwenye Sega la asali
 
Kama umempenda ondoka naye. Nenda naye ukatangaze kufunga ndoa. Ndoa itatangazwa kwa siku 21. Asipotokea wa kuweka zuio ndoa yenu kufungwa, then utakuwa mume halali wa huyo dada iwapo mtaoana.
 
Huyu hawajui wanawake wakidarisalama watch out!!!
 
Alisema aliyekuwa anasimamia mambo yao ya kuoana ni kaka yake mwanaume ambaye ni shemeji yake na amewahi kwenda kulalamika jinsi mwanaume alivyomtelekeza,kumbe shemeji ni ndugu wa kufahamiana kazini sio ndugu kabisa na mawasiliano na jamaa hana kwa sasa
 
Basi hana ndoa tena, alikutana na tapeli tu
 
Hili kwamba ni mke wa mtu umeligundua baada ya kutaka kuondoka ama? Unavyoelezea ni kama vile haukujua kama ni mke wa mtu kipindi chote mlichokuwa nae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…