Anaomba tuachane na sio kutengana!

rudi shule dogo!
 
Pole sana. Ila nimesoma message yako nikagundua kuwa mpenzi wako alikuwa anapata usumbufu toka kwa wanawake wengine sababu ya kuwa na wewe. Sasa hata ukipata mwingine ataishia kuwa na mateso alokuwa anapata huyu wa sasa. Cha kujiuliza ni nani hao wanaotuma message kwa mpenzi wako? Mimi kwa kweli niko upande wa huyo dada nisingependa kuolewa na mwanaume ambaye naanza kupata presha kabla sijaingia ndani. Wambie hao marafiki zako wa kike wawe na heshima kwa wapenzi wako otherwise utaachwa kila siku hasa ukipata mdada anayejiamini hawezi kuvumilia upuuzi wakati wewe si mume wake. I would do the same.

Na unaposema kuwa anakutesa unakosea ni wewe ndio unaemtesa. Angekuwa amekuacha bila sababu ningesema anakutesa. Lakini kama kutwa anapokea message za hajabu hajabu ya nini ajiingize kwenye ndoa na mtu wa design yako.
 
Reactions: F12
Thanks members, naamini mawazo yenu yakinifu ni mwongozo wangu kuelekea mafanikio, labda haikua riziki yangu na yeye hakunifikiria kwa future. Namtakia maisha mema na huyo mpya wake mwenye penzi lisilo na mateso, lakini daima ukitenda haki na Mungu atakubariki.

Don't take life so serious, it isn't permanent!
 
u ar better off without her! MJ1 amenena. hata mfunge ndoa kama ni kuishi kwa sms mbona mtateseka sana? na watu wakiwajua watawashughulisha kweli! akikua ataelewa, muambie ukweli ulivyo then muache aamue. usibaki kuwa nae kwa kumlazimisha ama kumn'ang'ania. na usihofu kuhusu kutambulisha kwa wazazi, watu wamebadili mawazo wakati vikao vya harusi vishaanza na mahari zishalipwa, seuze nyie? ndoa ni commitment ya maisha, usifanye papara wala hofu. moyo una threshold ya maumivu ya hali ya juu,utapona na utapendwa tena hadi ushangae! keep busy,maisha lazma yaendelee kaka
 
nyumba kubwa,naomba kutofautiana na ww! hujawahi kuona wanawake wanamtongoza la'aziz wako tena kama wanataka wambake? aisee,kama ni maisha ya kusikiliza watu bila kufanya homework yako mtafika kweli? nadhani huyo dada angekaa na f12, wakajadili loop hole iko wapi. dada amewapa screw driver, hao madada watam-screw. maybe it was better ameondoka.manake relation ya 3 yrs na bado hajiamini,kha!
 
Duh pole...ila things happen for a reason so ni kuendelea na maisha na in time utasahau na utapata mwingine
 
Mimi naungana na nyumba kubwa!

Jichunguze; inawezekana kuna shida kubwa sana upande wako, either u were a player or u r still one! Kama kulikuwa na shida huko nyuma, na umeamua kukaa naye; ni borakumuandaa kisaikolojia mwenzio ili ajue anapambana na nani/nini!

Naona wewe ulikuwa unadeny everything, huku mwenzio anapata maushahidi kibao!

Nikupe mfano halisi! Kuna jamaa alioa, then akaja kukutana na X wake wakaamua kukumbushia; kitu ikanasa (mimba). Sasa huyo X akatimia hiyo kitu kuharibu ndoa ya jamaa, akamfuata mke wa jamaa matusi na kejeli kibao! Jamaa kurudi anamkuta mkewe kavomba Uso kwa kilio, alivyosimuliwa jamaa akanpigia Simu X aje home! Jamaa na mkewe wakamtukana na kumtimua Yule X akaondoka kwa aibu!

Mwanaume alivyoside kwa mkewe, ndoa iliimarika badala ya kuvunjika!

Kwa hiyo ndugu yangu, sema tu Haruna jinsi ya kupata the other side of story; wewe ndie sababu ya uchumba went kufa!
 
nadhani huyo dada angekaa na f12, wakajadili loop hole iko wapi. dada amewapa screw driver, hao madada watam-screw. maybe it was better ameondoka.manake relation ya 3 yrs na bado hajiamini,kha!
<br />
<br />

What if huyo dada alikuwa anamuuliza huyo jamaa, na alikuwa anadeny tu?

What if hao wadada kweli wana uhusiano na huyo mkaka?

What if kaka was not strong enough to defend his love?

Angalia story yangu hapo juu, it is a real one, na mwanaume was guilty na aliadmit lkn good thing aliside kwa mkewe?
 

Si hivyo Nyumba Kubwa ila message kaipata 1 tu na ndio ilompa nguvu ya maamuzi ya kuniacha kadri ya maelezo yake pamoja na kuwa alikuwa akinieleza kwa hasira na jeuli.
 
Before mahusiano nliondoa tofauti zote za kimapenzi nlizokua nazo pia nae alifanya hivyo na tukaishi bila hofu yeyote kimapenzi lakini nadhani udhaifu wa moyo wake ulimfanya achukulie uzito kila neno analopewa na watu na keshaomba kuachana mara kadhaa kwa7bu ya maneno ya watu na akigundua kuwa sio kweli basi anarudi na mie bila kinyongo nampokea tena lakin kwa sasa kanambia tayari kampata mwingine na nisimpigie tena simu kujadili mapenzi labda mengineyo pamoja na kujibiwa jeuli kila nikipiga simu. Naumia zaidi nikikumbuka zile jitihada tulizokua tunafanya kwa lengo la kuandaa future kwan nlikua nafanya kwa moyo huku nikiamini nafanya kumfanikishia yule niliyempa hadhi ya kuwa Part of my body. Ila poa let it be kwan maumivu yatakwisha japo natoil ile mbaya.
 
Kama wewe huna tabia anayokulalamikia basi pia ni tatizo. Na hayo maneno ya watu yanatoka wapi? Ni watu gani? Inabidi uwajue ili uwatolee uvivu maana watakuharibia all your future relationships. Ukishajua maneno walyomwambia mpaka yakamfanya abwage manyanga; jipange ukimpata mpenzi mpya mwambie yote ili wakija kumwambia isiwe suprise.
 
Reactions: F12
Wadada wa hivyo nawatamani kweli niwafundishe adabu kama hawakufundwa kwao. Haijawahi kunitokea hiyo aisee. Labda message ilopotea njia. Yani nikujue kabisa sijuhi unafanya kazi na hubby afu unitumie message za kipuuzi ntakushughulikia kwa nguvu zangu zote. Uzuri napenda sana kesi.
 
<br />
<br />
Unapenda sana kesi we mpare nini?manake wapare kwa kupenda kesi ni nouma
 
ukweli kupenda kunatofautiana hasa unapopata uliye mpenda ila yeye hakupendi ni aibu na maumivi sana ndani ya roho
 
Reactions: F12
Pole sana! hakupendi huyo, akupendaye angefight for u. achana nae yupo wako akupendaye, msubiri, kabiliana na ishu ya taarifa kwa wazazi wewe si wa kwanza, na wala si tatizo kubwa.
 
Reactions: F12


Ni PM mie niko single tena natafuta mwenza.
 
Reactions: F12
Jibidishe ktk shughuli zako jiongezee kipato zaidi and forget about the lady always mawazo yao si ya mbali atajuta muhimu mwanaume yoyote yule jiweke kuwa bora wanawake wapo wengi atakuja wa dhati
 
Pole kaka,dada huyo hajapenda kama angekuwa kapenda kwa dhati asingekimbilia muachane..amempata wapi huyo jamaa mwengine wakati ulikuwa na uhusiano naye?so amekusaliti kuwa na mtu wakati yuko na wewe,huyo dada alikuwa amekuweka kwenye mzani ili ajue kati yako na huyo mwingine ni nani anamfaa so akaona wewe hukidhi viwango vyake ndomana anatafuta sababu ili muachane.achana naye.
 
Reactions: F12

Wawili wakipambanishwa lazima mmoja ashindwe so kwa hapa nadhani mimi ndio ilikuwa kiama changu. Mungu humpa mtu kadri ya makusudi yake na jinsi alivyompendeza kwa matendo yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…