Anaomba ushauri kuhusu talaka na haki ya kupata watoto wake!

Anaomba ushauri kuhusu talaka na haki ya kupata watoto wake!

BornTown

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2008
Posts
1,716
Reaction score
482
Nimeombwa ushauri na rafiki yangu mmoja nimekosa jibu la kumpa issue yenye iko hivi:

Ni mkaka wa miaka 40 alikuwa na mahusiano na mdada mmoja wakaja wakaachana kutokana na huyo mkaka kupata mwanamke mwingine ka kipindi cha miezi 3 cha urafiki mpya na huyo mwanamke mwingine wakafunga ndoa kanisa katoliki waliishi mwakamiaka 2 na nusu wakakorofishana.

Hapo walijaliwa kupata mtoto wa kike na wakiume baada ya kukorofishana mwanamama akakimbilia kwako anadai chanzo ni wivu wa mke kupitiliza mke hataki baba aongee na mwanamke yeyote yule hata kazini kwa baba asizungumze na mwanamke hata kama wanafanya wote kazi.

Ukija mtaani mama hataki mahusiano na wenzie akiona mama wa jirani akimsalimia mumewe ni ugomvi sasa alicho kifanya akavuruga pale mtaani kwake hivi anamfuata mke wa jirani anamwambia mumeo kanitongoza halafu anaenda kwa mume anamwambia mkeo anatembea na mume wangu.

Ikumbukwe anafanya hivyo kwa kila familia pale mtaani kwao alifanya hivyo kwa majirani zake karibu 10 ss ukawa ugomvi mke anamtuhumu mume na mume anamtuhumu mke.

Mwisho wasiku wanaume wakaitana wakaa wakaamua kumwita huyu kaka wampe kubwa walipanga kumfanyia kitu mbaya sana huyo kaka wakiamini kuwa ni kweli anatembea na wake zao.

Sasa basi wakati wanayapanga hayo yule kaka tokea kwenye ile bar waliokaa akawasalimia hakuna aliye mjibu akawashangaa jirani zake wamekuwaje akamfuata mmoja ambaye ni mkubwa kuliko wote ni mtu mzima akamwambia mzee nina shida nataka kukueleza jambo.

Basi yule baba akamsililiza yule kaka akamwambia mkewe anamtuhumu mambo ambayo hayawahi kuyafanya na wala hategemei kuyafanya pale mtaani wanaume wakakaa wakayaongea wakakubalia jmosi inayofuata jumuiya inafanyika kwa huyo mkaka basi watakaa wayaongee.

Wakarudi majumbani mwao kila mtu akamweleza mkewe kuwa jmosi tutayamaliza maneno yote tukitoka jumuiya. Mmoja wa hao kinamama akamfuata mke wa huku kaka akamweleza kuwa jmosi tunakuja kukata mzizi wa fitina.

Mke kuambiwa hivyo akatahamaki akasubiri mgeni ametoka akapiga simu kwao akaita kenta akasomba kila kitu akakimbilia kwao mume kurudi jioni nyumba nyeupe kama wanataka kuhamia akipiga simu ya mkewe haipokelewi akawauliza majirani wamakwambia mkeo ndie alihamisha vitu.

Basi kaka wa watu akaenda nyumbani kwa wakwe zake kumfuata mke kujua tatizo akafika na kupokelewa na matusi mama na baba mkwe wanamtukana kuwa amepanga yeye na jirani zake kwenda kumuua binti yao.

Uzuri yule kaka alitoka na yule mzee mtaani kwake ili amsindikize yule baba alishangaa kusikia yale maneno toka kwa wale wazee. Akajaribu kuwaeleza wale wazee walichofanya ni kuwafungulia mbwa na kuwaitia makelele ya wezi wakakimbia kunusuru maisha yao.

Hadi sasa ni mwaka wa 4 unaenda yule dada hajarudi kwa mume na hataki mume awaone watoto. Sasa ushauri anaomba ni

Je akienda mahakamani huyu kaka kudai talaka na apate haki ya kukaa wa watoto wake

Pili ili aoe tena na je kanisa katoliki litamruhusu kufunga tena ndoa kanisani?

Sheria inachukua muda gani kutoa talaka maana ngazi zote ameshapitia ustawi wa jamii imeshindikana mabaraza ya wazee nao imeshindikana aombeni ushauri nimsaidieje.
 
Hawezi kuoa tena kanisani maana sis wakristo tunaamini kifo ndio kinatenganisha ,kuhusu watoto kama wana miaka 7 na kuendelea aende mahakamani afungue kesi atashinda na watoto atawachukua,pole yake maana kweli alipata mke loo hatari kweli kweli.
 
Kuna habari nyingi zinakosekana katika stori yako ila kiufupi ni hivi:

Kuhusu yeye kwenda mahakamani ni haki yake na hazuiwi na yeyote, ndoa aliingia mwenyewe kwa hiari yake na akitaka kutoka hakuna wa kumzuia huko.

Hao watoto itategemea mambo mengi mojawapo ikiwa ni umri wao kwa sasa.

Sijaelewa unavyouliza kuhusu "sheria inachukua muda gani kutoa talaka" ni swali tata kidogo na haliwezi jibika labda ufafanue.

Ukiuliza habari ya kanisa katoliki humu Jukwaa la sheria unatuonea maana naamini wengi wetu sio makasisi, wala mapadri labda kama wapo humu mapadri wanasheria.

Japo naweza kujibu "kirahisi" kwamba kiapo cha ndoa kinasema hadi kifo kitakapo tutenganisha kwamaana ya kwamba baada ya kifo cha mmoja wao hawatahesabiwa tena kuwa mume na mke hivyo aliebakia anaweza oa ama kuolewa, sasa sijui kama kutengana kunaweza ingia ndani ya tafsiri ya neno kifo ama kama kunataratibu gani pale wawili wanapotengana.
 
@Mapi , Asante watoto bado ni wadogo miaka 4 kwa 6 anataka kuwa na access ya kukaa nao even wkend maana wakwe zake na huyo mke hawataki awaone watoto kabisa ingawa pesa ya matumizi ya wanae anapeleka kila mwezi laki 3 tena anadeposi kwenye account ya huyo mke na risiti anaweka shule alio waandikisha watoto mke kakataa kuwapeleka wanasoma shule za mtaani. kwa miaka 4 hajaona wanae kabisa hilo ndilo linalomuumiza zaidi. Suala la kuoa amechoka maisha ya kuwa mpweke.
 
hawezi kuoa tena kanisani maana sis wakristo tunaamini kifo ndio kinatenganisha ,kuhusu watoto kama wana miaka 7 na kuendelea aende mahakamani afungue kesi atashinda na watoto atawachukua,pole yake maana kweli alipata mke loo hatari kweli kweli

Asante wa ushauri ila nasikia sikuhizi wanakubali kuvunja ndoa na kufungisha ndoa nyingine ili kuwaondoa watu kwenye uzinzi maana kuishi na mke bila ndoa nayenyewe ni dhambi ya uzinzi
 
asante wa ushauri ila nasikia sikuhizi wanakubali kuvunja ndoa na kufungisha ndoa nyingine ili kuwaondoa watu kwenye uzinzi maana kuishi na mke bila ndoa nayenyewe ni dhambi ya uzinzi
si kweli kabisa na hairuhusiwi labda huyo jamaa aishi na mke na ikijulikana kanisani basi mtaonekana ni wazifu
 
Asante watoto bado ni wadogo miaka 4 kwa 6 anataka kuwa na access ya kukaa nao even wkend maana wakwe zake na huyo mke hawataki awaone watoto kabisa ingawa pesa ya matumizi ya wanae anapeleka kila mwezi laki 3 tena anadeposi kwenye account ya huyo mke na risiti anaweka shule alio waandikisha watoto mke kakataa kuwapeleka wanasoma shule za mtaani. kwa miaka 4 hajaona wanae kabisa hilo ndilo linalomuumiza zaidi. Suala la kuoa amechoka maisha ya kuwa mpweke
ni wewe unaelekea kuolewa nae nini? (Utani)

cha msingi afungue shauri mahakani la kudai talaka na katika shauri hilo hilo pia aombe kuishi na watoto (maamuzi yatabaki kwa mahakama) ila akiweza kuishawishi mahakama kwamba mama hana uwezo wa kuwatunza watoto na kwamba mama anamnyima kuona watoto wake na pia mama hana lengo zuri na elimu ya watoto kwa kuwapeleka kwenye shule hizo nyingine (pengine ubora mdogo) kulinganisha na huko anakolipia ada ila watoto hawappelekwi mahakama inaweza mpa nafasi hiyo
 
Asante watoto bado ni wadogo miaka 4 kwa 6 anataka kuwa na access ya kukaa nao even wkend maana wakwe zake na huyo mke hawataki awaone watoto kabisa ingawa pesa ya matumizi ya wanae anapeleka kila mwezi laki 3 tena anadeposi kwenye account ya huyo mke na risiti anaweka shule alio waandikisha watoto mke kakataa kuwapeleka wanasoma shule za mtaani. kwa miaka 4 hajaona wanae kabisa hilo ndilo linalomuumiza zaidi. Suala la kuoa amechoka maisha ya kuwa mpweke

Sina ushauri wa kisheria.

Ila huyo mume tatizo kalilea kiufupi yeye ndio anampa mke jeuri.

Mke ana uhakika wa laki 3 kila mwezi.

Angezisitisha hizi wangemtafuta wenyewe
 
Sina ushauri wa kisheria.

Ila huyo mume tatizo kalilea kiufupi yeye ndio anampa mke jeuri.

Mke ana uhakika wa laki 3 kila mwezi.

Angezisitisha hizi wangemtafuta wenyewe
Tatizo anawaonea huruma watoto wake ila nashukuru kwa ushauri wenu nyote nimeikusanya na nitamweleza hapo itakuwa akili kumkichwa kwake asuke au anyowe.
 
Hapo naona amtafute tu huyo dada wakasuluhishwe huko kanisani? Hakuna ndoa inayovunjika sababu ya wivu...
Story yako ni ndefu sana... watoto wanaishi na nani?
 
Je akienda mahakamani huyu kaka kudai talaka na apate haki ya kukaa wa watoto wake

Pili ili aoe tena na je kanisa katoliki litamruhusu kufunga tena ndoa kanisani?

Sheria inachukua muda gani kutoa talaka maana ngazi zote ameshapitia ustawi wa jamii imeshindikana mabaraza ya wazee nao imeshindikana aombeni ushauri nimsaidieje.

Look! Si kazi ya Idara ya Ustawi wa jamii wala Mabaraza ya Wazee kushulikia mambo ya talaka (divorce). Masuala ya talaka hushughulikiwa na mahakama baada ya mdai talaka (ambapo peningine anaweza kuwa huyo kaka) kwenda kufungua shauri la madai ya talaka katika mahakama.

Mahakama ndio hutoa (summons) au hati ya mdaiwa kufika mahakamani (summons) kusikiliza shauri la madai. Na pengine sasa hapo angeweza kuwa huyo dada sasa, iwapo tu huyo kaka angekwenda ku faili shauri au kesi ya madai ya talaka . Ni katika hiyo process ya usikilizaji wa shauri la madai ya talaka masuala ya watoto na pengine kumiliki mali zilizochumwa na wanandoa kwa pamoja yangeibuka na kutolewa ufumbuzi na hakimu.

Baada ya hakimu kusikiliza taarifa za pande zote mbili ndio hapo huhitimisha shauri kwa kutoa hati ya talaka (Divorce certificate) pamoja na angalizo la talaka (Divorce decree) ambalo ni maagizo juu watoto (taarifa za kama vile nani ana stahiki ya kuishi nao au kulipa gharama za malezi ya watoto (yaani child support) na mengineyo juu ya mgawanyo wa mali (yaani kama zipo zilizochumwa pamoja).

Huo ndio mchakato wa kudai talaka ambao rafiki yako anapaswa kuufuata na si vinginevyo kwani hakuna mkato. Kwa kanuni za kanisa halitoi wala kubariki talaka. Kuhusu suala la kurudi tena kuoa kanisa katoliki asahau tu. Bali anaweza funga ndoa kwa RC (bomani) bila shida au hata ndoa kijadi.

Kwa mujibu wa ufahamu wangu wa kisheria naamini nimekujibu.
 
Amuulize Dr.W.Slaa daktari wa kanoni aliwezaje kuvuka vizingiti vya kanisa akazaa na wanawake zaidi ya mmoja. Au itakuwa na yeye hana ndoa hata moja ni mzinzi tu?
 
Last edited by a moderator:
Nabii mweusi@sawa lakini ,hivi hiyo ndoa haina washeng?Mleta mada naye ni tutusa na hatachukua ushauri hata tukimpa,mods futa huu uzi,alipofunga ndoa kazi ya washenga ni kufuta jasho tu?Hivi ama ni ndoa za utotoni?Ama hii story ni ya shigongo ambayo naye katafsiri toka vitabu vya James Hadley Chase?
 
Asanteni kwa ushauri wenu amejitahidi kutafuta usuluhishi kwa mkewe kwa miaka minne bila mafanikio ameshatumia wazee wa pande zote mama hataki amekwenda vilevile kanisani imeshindikana mama hataki kurudi kwake aliondoka mwenyewe bila kufukuzwa na watoto mume amechoka kwani hata hapewi watoto wake awaone japo hata nusu saa ya kuwa nao ustawi wajamii wameshamuita huyo mama hataki kwenda. Mume akatafuta shule akalipia mama hajawapeleka watoto ada imepotea bure na anataka matumizi ya watoto kila mwezi kuna duka alifunguliwa kubwa tu kipindi wanaishi wote mama amelifunga amelihamisha. Akataka kutoroka na watoto aende nje ikashindikana kwani alikwamia uhamiaji kuna marafiki wa mume walimshtua jamaa kuwa mkeo kaenda kuwakatia watoto passports.

Mume amekwenda mahakamani kufungua madai ya kutalikiana na mkewe na apate haki ya wanae
 
Back
Top Bottom