Anapenda kufanya kazi inayomlipa kutokana na kujituma kwake; Je, asomee taaluma gani?

Mshua's

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Posts
804
Reaction score
553
Wakuu habari zenu!

Kuna kijana amemaliza form 6 amekuja kuniomba ushauri kuwa asomee taaluma gani ambayo itamuwezesha kufanya kazi ikiwa mapato/malipo yanategemea na kujituma kwake/bidii kazini. Malipo hayo yawe yanafanyika mara anapokuwa amemaliza kufanya kazi husika aidha baada ya siku kadhaa na siyo kwa mwezi!

Nimeona niwashirikishe ili muweze kutoa michango yenu inayoweza kumsaidia huyu kijana. Binafsi sijaona kazi ya aina hiyo kwa hapa Tanzania.

Mshua
 
Hiyo kazi hapa Tanzania ipo nayo ni kujiajiri, atafute mtaji tu atumie elimu yake kujizalishia badala ya kuzalishia wengine.
 
Hiyo kazi hapa Tanzania ipo nayo ni kujiajiri, atafute mtaji tu atumie elimu yake kujizalishia badala ya kuzalishia wengine.

Biashara anaweza kukaa hadi wiki hujauza kama akikosea kwenye uchaguzi wa biashara ya kufanya ndiyo basi tena! Anamaanisha kazi inayopimika ya kiofisi yaani, kadri unavyomaliza kipimo hicho haraka, unaongeza kipimo kingine ili kuongeza kipato. Ndiyo maana nikasema Tanzania hakuna
 
Sasa hivi ni hasara tupu kuwasomesha hawa watoto, ni kwa nini wewe au yeye asifikirie kuajili watu wa kumzalishia na anawaza kuajiliwa tu. janga.
 
Kazi yeyote ile ila siyo ualimu !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…