Anapenda kukata tamaa mapema

Anapenda kukata tamaa mapema

marida

Senior Member
Joined
Oct 27, 2011
Posts
168
Reaction score
20
Habari zenu wana jf.Nina rafiki yangu wa kiume,huu mwaka sasa unakata,tupo marafik vizuri tu,tatizo alilonalo,hajui kumtongoza mwanamke..eti yeye anasema action atakazokuwa anaonyesha kwa
yule ampendae atajua tu mwenyewe,kashawahi kukutana na mabinti kama 6,lakini kutokana na kutojiexpress mwenyewe anataka nini kutoka kwa hao mabinti,anashindwa kabisa,ingawa wapo waliojiongeza na kujua anataka nini kutoka kwao,ila hawawezi kumtamkia chochote,na yeye yupo kimnya tu,anaumia moyoni..
Sasa juzi juzi kakutana na binti mmoja,wamekuwa marafiki kwa muda wa miezi 5,kampenda kweli,tatizo hawezi mtamkia kabisa,they end up discussing mada ambazo ni unnecessary,na msichana anamchukulia kama anavyojileta kwake,akimpa story za shule,nae analeta za shule,za nyumban nae anaongelea hayo hayo.Mwisho,anaconclude mwenyewe eti hanipendi,Jamani huyu ndugu yangu anamatatizo gani?,ni kwamba hawezi kumtamkia mwanamke nakupenda au ni ugonjwa?.Sometimes utakuta ananiambia marida,leo lazima nimwambie ukweli nampenda,akifika kule,ananywea huyo.Nikija kumuuliza baadae,anasema hanipendi yule msichana,huku akihuzunika..

Kama kifamilia,kwao wote ni wavulana,sijui ni hali ya kawaida tu kwa mvulana yoyote kutokea hivyo?.Help this friend of my mine please!by your good ideas.

Tatizo ni nini?
 
Ni rafiki yako wa kiume! kama wewe umemwelewa udhaifu wake si umkubali ww mambo yaishe! atakuwa mume mzuri mbeleni kwani, domo zege lake litakupa uhuru wa kujihamini jamaa akiwa mbali na ww.
 
Hajapenda kweli huyu,akipenda hasa ndani ya moyo wake atasema utashangaa.
 
msaada unaweza kumpa wewe mwenyewe.kwa opc 2 moja unaweza kumpigia sound kwa huyo dem.kwakumwambia live huyo dem kua jamaa anampenda ila ameshindwa kumwambia.au kwa kuwaambia wote wakiwa 2 mfano unaweza kuwatania kua wanapendeza kama wangekua mke na mume.hapo utakua umempa jamaa njia ya kuanzia
 
muongoze ajiunge JF wamfundishe hapa atapata PHD kabisa
 
msaada unaweza kumpa wewe mwenyewe.kwa opc 2 moja unaweza kumpigia sound kwa huyo dem.kwakumwambia live huyo dem kua jamaa anampenda ila ameshindwa kumwambia.au kwa kuwaambia wote wakiwa 2 mfano unaweza kuwatania kua wanapendeza kama wangekua mke na mume.hapo utakua umempa jamaa njia ya kuanzia

Umemaliza, hii nimeipenda
 
labda si rizki.... kama vipi hebu check nae uone kama anapanda mtungi...
 
msaada unaweza kumpa wewe mwenyewe.kwa opc 2 moja unaweza kumpigia sound kwa huyo dem.kwakumwambia live huyo dem kua jamaa anampenda ila ameshindwa kumwambia.au kwa kuwaambia wote wakiwa 2 mfano unaweza kuwatania kua wanapendeza kama wangekua mke na mume.hapo utakua umempa jamaa njia ya kuanzia
Utamuunganishia jamaa namna hiyo, lakini akifika eneo la tukio huoni kwamba itakuwa ni kituko?
Jamaa atashindwa jinsi ya kuanza kupakua juis ambayo tayari iko kwenye jagi!...huh!
 
Rainforced Concrete huyo,

Ajaribu kuwazoea hawa wenzentu, mfano awe na mazoea yakuwasalimia warembo akikutananao kwa road, ajipe hiyo assignment na pia ajichanganye nao ili awazoee, naamini ataweza tu.. Asitumie sana Non verbal communication...
 
Utamuunganishia jamaa namna hiyo, lakini akifika eneo la tukio huoni kwamba itakuwa ni kituko?
Jamaa atashindwa jinsi ya kuanza kupakua juis ambayo tayari iko kwenye jagi!...huh!

Kumbe juis yapakuliwa?
 
Anatakiwa ajiamini kwanza, huenda anaogopa kutongoza kwa kuhofia kutolewa nje. Ila bado unayo nafasi ya kumwongoza namna ambavyo anaweza kuji express kwa wadada maana kutongoza ni zaidi ya kusema unampenda msichana.
Huo mtizamo wake wa action unaweza kufanikiwa lakini utachukua muda sana na inategemea na aina ya mdada.
 
Habari zenu wana jf.Nina rafiki yangu wa kiume,huu mwaka sasa unakata,tupo marafik vizuri tu,tatizo alilonalo,hajui kumtongoza mwanamke..eti yeye anasema action atakazokuwa anaonyesha kwa
yule ampendae atajua tu mwenyewe,kashawahi kukutana na mabinti kama 6,lakini kutokana na kutojiexpress mwenyewe anataka nini kutoka kwa hao mabinti,anashindwa kabisa,ingawa wapo waliojiongeza na kujua anataka nini kutoka kwao,ila hawawezi kumtamkia chochote,na yeye yupo kimnya tu,anaumia moyoni..
Sasa juzi juzi kakutana na binti mmoja,wamekuwa marafiki kwa muda wa miezi 5,kampenda kweli,tatizo hawezi mtamkia kabisa,they end up discussing mada ambazo ni unnecessary,na msichana anamchukulia kama anavyojileta kwake,akimpa story za shule,nae analeta za shule,za nyumban nae anaongelea hayo hayo.Mwisho,anaconclude mwenyewe eti hanipendi,Jamani huyu ndugu yangu anamatatizo gani?,ni kwamba hawezi kumtamkia mwanamke nakupenda au ni ugonjwa?.Sometimes utakuta ananiambia marida,leo lazima nimwambie ukweli nampenda,akifika kule,ananywea huyo.Nikija kumuuliza baadae,anasema hanipendi yule msichana,huku akihuzunika..

Kama kifamilia,kwao wote ni wavulana,sijui ni hali ya kawaida tu kwa mvulana yoyote kutokea hivyo?.Help this friend of my mine please!by your good ideas.

Tatizo ni nini?

Marida,

Tafadhali usimwangushe. Kama anatafuta mke msaidie apeleke posa. Kama anatafuta msichana wa kumchezea (mpenzi?) si vizuri kufanya hivyo. Bora alivyo na kigugumizi kuliko kuwa kiwembe. Tafadhali asianze mapenzi kabla ya kuoa.
 
naomba unipm nikupe maelezo kuna dawa bib yng anayo ukimywa tu zege lote linayeyuka kitu kinakua ka cherehan vle.
 
Kweli mzima rafiki yako na wasiwasi nae sana au mpaka kilabu kidogo ndo ataweza kunena
 
Back
Top Bottom