Anaripoti Askofu Mwamakula hakika nchi hii % kubwa watu wamekuwa zaidi ya wanyama

Anaripoti Askofu Mwamakula hakika nchi hii % kubwa watu wamekuwa zaidi ya wanyama

Pozzers

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
337
Reaction score
560
Anaripoti Askofu Mwamakula hakika nchi hii % kubwa watu wamekuwa zaidi ya wanyama.

Tunaomba Rais akemee watu wake hawa maana yeye ndo mkuu wao kuanzia utumishi na wazazi wenye watoto wa kike tusiruhusu waende huko huo ni uuaji kama uaji mwingine. BINTI ALIYELALA NA WANAJESHI AJILIPUA!

Kuna sauti (voice mail) inasambaa mitandaoni. Ni ya binti ambaye hajajitambulisha jina lake ila anamueleza rafiki yake aitwaye Irene akimtaka asithubutu kwenda JKT!

Hoja yake kuu ni kuwa wasichana wakiwa JKT wanalazimishwa kulala na wanajeshi kinyume cha matakwa yao.

Huyo binti anasema yeye alilala na wanajeshi watatu ingawa anasema wengine walilala na wanajeshi wengi zaidi.

Anasema wapo waliorejea wakiwa na HIV positive.

Anasema msichana akikataa kufanya mapenzi anapewa adhabu nzito, hivyo ili kujiponya ni lazima awakubalie matakwa yao.

Anasema leo akija huyu, siku nyingine atakuja mwingine na mwingine hadi uwe sugu.

Voice mail hiyo imezua taharuki kubwa kwa wazazi walio na watoto wa kike wanaotarajiwa kwenda JKT mwaka huu.

Mmoja wa wazazi ambaye ana jina kubwa nchini ametuomba ili tulipazie sauti jambo hili.

Kwa sasa sauti hiyo inazunguka na kujadiliwa kwenye magrupu ya Wasapu.

Ni sauti iliyovuja pengine bila hata ya idhini ya mtoa sauti na mlengwa.

Hatuwezi kuzuia binti zetu wote kwenda JKT. Kanuni ya Task consent inawataka watumikie taifa lao ambapo JKT ni sehemu ya utumishi huo wa Taifa.

Hata hivyo hofu, madai na hata malalamiko hayo siyo ya kuyapuuzia kbs.

Sisi maaskofu tunafahamiana na watu walioshika nafasi kubwa kabisa JKT na JWTZ miaka ya hivi karibuni. Hivyo tunatambua kuwa hiyo ya kulazimisha ngono kwa mabinti sio sera ya majeshi yetu bali ni ukorofi wa baadhi ya askari kwa visingizio visivyo kuwa na maana.

Kwa sababu hiyo, tunatoa wito kwa Mkuu wa JKT kutoa kauli ya kuwakikishia wazazi kuwa binti zao watakuwa salama lakini pia kuwaonya wanajeshi makambini kuwa atakayepatikana na kosa hilo atafukuzwa kazi.

Zaidi ya yote, kila Kambi ya JKT iwe na dawati la malalamiko ya wasichana ili kila siku lipokee malalamiko na wasichana waruhisiwe kutaja majina au namba za wanajeshi wanaowasumbua kingono!

Kama tutashindwa kuyadhibiti matendo hayo katika makambi ya JKT basi pengine iwepo pia haja ya kuanzisha Kambi za Wanawake peke yao.

Tunaamini kuwa andiko hili litawafanya Wakuu wa JKT kutoka hadharani kuwatia moyo mabinti na wazazi kuwahakikishia usalama.

Sisi maaskofu tutaanza kupeleka watu katika hayo makambi ili kama kuna matukio ya unyanyasaji wa kingono kwa mabinti tuyaweke hadharani.

Ni kosa kumlazimisha mtu kufanya mapenzi bila ya ridhaa yake. Watu wachache wasiharibu JKT tukiwa tunawatazama!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 1 Juni 2023.
 
Wanajeshi nchi za afrika wengi wao akili ndogo, wanatumia nguvu na ubabe ila akili hayana ukitaka kujua hilo chunguza kesi ya ugaida ya mbowe utajua hili.

Nchi za wenzetu ulaya na marekani wanajeshi ni mnyonge kuliko raia tena wanapiga mpaka magoti kuomba msamaha rejea kwenye maandamano ya kifo cha George Froyd.

Wanajeshi jitambueni zama zimebadilika raia ni watu hatari sana wakiamua, muulizeni Omar AL bashir na jeshi lake saizi ananyea ndoo Sasa wewe askari wa Jkt kinda kabisa unaleta usela Mavi
 
Lazima guarantee itolewe kwa wazazi hasa wa watoto wa kike ili wawe na uhakika na usalama wa watoto wao. Maana tunaambiwa jeshini huwezi kugomea amri ya kamanda, sasa itakuwaje ikiwa amri hiyo itataka apewe ngono bila hiari ya mhusika? Vinginevyo serikali iweke utaratibu mzuri kabla ya kufanya haya mafunzo kuwa ya lazima kwa wahitimu wote.
 
La sivyo wasichana iwe hiari yao kwenda au kutokwenda JKT
Kwa kweli kama ni hivyo basi na wepewe immunity
 
Wanajeshi nchi za afrika wengi wao akili ndogo, wanatumia nguvu na ubabe ila akili hayana ukitaka kujua hilo chunguza kesi ya ugaida ya mbowe utajua hili. Nchi za wenzetu ulaya na marekani wanajeshi ni mnyonge kuliko raia tena wanapiga mpaka magoti kuomba msamaha rejea kwenye maandamano ya kifo cha George Froyd.

Wanajeshi jitambueni zama zimebadilika raia ni watu hatari sana wakiamua, muulizeni Omar AL bashir na jeshi lake saizi ananyea ndoo Sasa wewe askari wa Jkt kinda kabisa unaleta usela Mavi
Peleka binti yako akapewe elimu ya kijeshi utamla wewe
 
Mzazi ukiruhusu mtoto wako aende huko, wewe mzazi huna akili.

Wahindi na Waarabu watoto wao wapo madukani wakijifunza biashara, wewe unapeleka mwanao akalime nyanya,
 
Back
Top Bottom