Anasimulia Mwanachama Wa Simba na Ambae aliwahi kufanya Kazi Kwenye Makampuni Mohammed Dewji

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Naomba nikiri mimi ni Mwanachama wa Simba na nilishwahi kufanya kazi kwenye moja ya makampuni ya huyu anayejiita YOUNG BILLIONAIRE (si lolote si chochote).

Niliwahi fanya kwenye kampuni ya 21st CENTURY, kisha mkataba wangu ukaamishiwa kampuni la EAST COAST akaniamishia tena mkataba wangu kwenye kampuni ya ROYAL DETERGENTS kote huko lengo ni kupunja maslahi yangu ajira ya mwanzoni.

Kwa msiomjua Mo -Dewji na hujawahi kufanya kazi kwenye makampuni yake au kwenye taasisi zake unaweza kumlaumu Mzungu na unaweza kupuuza yale malalamiko ya Haji Manara wakati alipolalamika alivyofanya kazi na Bw. Mo.

Kwa kifupi Mo-Dewji ni mnyanyasaji mkubwa wa wafanyakazi wake na mtu asiyefuata sheria za mikataba ya kazi.

Kwa makampuni ya Mo uwa hafukuzi wafanyakazi pale anapokuchoka anatumia watendaji wake kuanzisha hila na chokochoko ili uondoke mwenyewe na aminye haki zako za msingi.!

Limenitokea mimi, limemtokea Haji Manara na linamtokea mzungu.

Kwanza siku Manara aliposema alikuwa analipwa 700k nilishangaa sana mimi kumzidi mshahara, nilikuwa nalipwa 800k Kwa,Mwezi.

Yaani mimi wa kumzidi Manara mshahara wakati,Manara alifanya kazi Closed na Bwana Mo-Dewji.

Mshahara wangu ulishuka kutoka 1.5m mpaka 750k,kila nilipoamishiwa kampuni na kuanza upya mkataba wa ajira,nilishtuka nikaondoka kwa style ya MZUNGU.

KUHUSU KUCHANJWA MZUNGU
Sina hakika kama ameongea hivyo.KAMA NI KWELI alisema hayo,sishangai,kwani hata mimi wakati nafanya kwa Bw.Mo ,ilikuwa ni kawaida kuvunjwa nazi viwandani zenye maandishi ya kiarabu na tulilishwa vipande hivyo vya nazi.

Na ilikuwa ni LAZIMA ukikataa huna kazi au alichinjwa Mwanakondoo kwenye geti kuu la viwanda na nyama tuligawiwa.!

Kwa hiyo yote kwa yote yanawezekana.
 
Kama kuna kula kondoo naomba nipelekwe na yule mtumishi tukale hao wanaojiita 🐑
 
Tatizo la miutopolo mipuuzi ikishazidiwa ma Miko ya vinyeo unakuja na hoja mfu za kumchafua mtu. Malalamiko yako Kama Yana ukweli je hapa ndo sehemu sahihi pa kuyatatua au ni umbea tu?!
 
Kwa maelezo haya ni kuwa huyu mfanyakazi alikuwa hasaidii kampuni kukuwa. Yaani ukiona mshahara unapungua ni wazi utendaji wako ni mbovu.

Pili ni dhahiri anasema uongo mtupu maana haya yote kasubiri mzungu ameondoka ndio na yeye akakumbuka aifanya kazi kwa Mo.

Tatu, kama aliona haki zake zimeminywa alikuwa anaweza kwenda CMA kudai haki zake bali yeye akakimbilia kuacha kazi, tena akiwa na mkataba wa kazi.

Kwa kifupi huu ni mwandiko wa Manara kabisa.
 
Mo Dewj mwenye wafakazi ambao yy binafsi hata hajui sura au majina yao aanze kukunyanyasa ww aliyekuajiri ku operate machine hapo kiwandani na zaidi zaidi alikuajiri bila hata kukuona na mpaka sasa pengine na ww hunawahi hata kuonanana nae face to face.
Tuache kuchafua watu
 
Mbona haujashukuru ulivyopokea hela zake kama mishahara kwa muda ukimfanyia kazi.Yeye aliona kazi na weye ulipata kipato cha kukuweka mjini.Muwe na shukrani.Siyo kutafuta tu kumtusi mtu.
 
mpiga vichwa siku ukipata akili nitag
 
Linguistic : " Nilikuwa nalipwa 800k Kwa Mwezi."

Linguistic : "
Mshahara wangu ulishuka kutoka 1.5m mpaka 750k.

Swali: Ulikuwa unalipwa kiasi gani?
 
Acha kazi badala ya kulalamika. Asubuhi tu nafasi yako itapokea maombi zaidi ya 1000
 
Mwaka 1992 niliwahi kupata kibarua kwenye ofisi za Mohamed Interprises zilizopo pugu road apo chang'ombe shughulizao kubwa walikua wakiuza vyombo vya majumbani na ku import mafuta ya kupigia (korie) naku export korosho, ufuta n.k
Nilikuta Kuna wafanyakazi Wana miaka mingi wanatumika bila kuajiriwa. Chakushangaza wanaajiliwa wa Pakistan ambao walikua hawana ujuzi wowote zaidi ya kuwa wasimamizi wa kazi.
Niliondoka pale nikiwaacha jamaa nilio wakuta wakimsubiri Waziri wa mambo ya ndani Agustine Mrema aingilie kati.
 
Linguistic : " Nilikuwa nalipwa 800k Kwa Mwezi."

Linguistic : "
Mshahara wangu ulishuka kutoka 1.5m mpaka 750k.

Swali: Ulikuwa unalipwa kiasi gani?
bangi mbaya sana mkuu alikuwa analipwa m 1.5 ikashuka 75 afu hapo 80 hapa kuna walakini maskini hajawahi kumwombea tajiri mema mda mwing anawaza kunyanyaswa hana lingne
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…