Anatafutwa Semeni Bundala

Anatafutwa Semeni Bundala

Eswa

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2012
Posts
231
Reaction score
617
Habarini wanajamvi.?.

Jana katika ziara ya kikazi kijiji cha Matanga - Kongwa Dodoma, nilikutana na huyu mama, katika maongezi yetu aliniomba kumsaidia kumtafuta binti yake anayeitwa SEMENI BUNDALA waliachana naye muda mrefu sana, baba wa mtoto anaitwa BUNDALA NDUNG'O MANYELE (Maarufu kama KAZIMOTO), alimwacha akiwa anakaa na baba yake katika kijiji cha Iramba kata ya Igumanoni mkoani Tabora na yeye kuhamia Dodoma.

Huyu mama anaitwa Dina Mnyepembe anakaa kijiji cha Matanga - Kongwa Dodoma.

Mawasiliano: 0628 93 61 81 au 0622 13 46 57, hiyo ni namba jirani yake. Kama zisipopatikana unaweza kunipigia kwa 0652 52 77 76.

Naomba tusaidiane kusambaza ujumbe huu ili Semeni Bundala akutane na mama yake.

Asanteni sana.
 
Weka picha kuna demu uku morogoro anaitwa semeni ni mnyamwezi sijawahi kumuuliza jina lake la pili pia anaweza kuwa yeye , skin color yake ni maji ya kunde
 
Weka picha kuna demu uku morogoro anaitwa semeni ni mnyamwezi sijawahi kumuuliza jina lake la pili pia anaweza kuwa yeye , skin color yake ni maji ya kunde
Kwa bahati mbaya sana mama yake hakuwa na picha yake, maana anasema alimuacha akiwa mdogo sana, labda niambatanishe picha ya mama yake. Shukrani
 
Attachments

  • IMG-20220719-WA0054.jpg
    IMG-20220719-WA0054.jpg
    114.1 KB · Views: 6
Unamuacha mtoto miaka mingi auna habari naye, bila shaka huyu ni mama wa hovyo
Ni rahisi kumhukumu hivyo pasipo kujua sababu hasa ilikuwa ni nini, kumbuka si rahisi kwa mama kumwacha mtoto wake.! Tusimhukumu ila tushirikiane kumuunganisha na binti yake 🙏
 
Ni rahisi kumhukumu hivyo pasipo kujua sababu hasa ilikuwa ni nini, kumbuka si rahisi kwa mama kumwacha mtoto wake.! Tusimhukumu ila tushirikiane kumuunganisha na binti yake 🙏
Mzazi unashindwaje kufuatilia maendeleo ya mwanao isitoshe ni mama, namuombea akutane na mwanae lakini sidhani kama mtoto atakua na mapenzi na mama ake.
 
Pole kwake mzazi huyu haya ndio matokeo ya kuishi in a pithole country, ID number ya huyu aliyepotea ingekuwa rahisi to trace na kuona last movement zake alikua wapi
 
Unamuacha mtoto miaka mingi auna habari naye, bila shaka huyu ni mama wa hovyo
Maisha yana changamoto nyingi sana mkuu,huwezi kujua kuna kitu gani kilijitokeza hadi akapata maamuzi ya kuhama mkoa.
Usihukumu kwa haraka hivyo
 
Maisha yana changamoto nyingi sana mkuu,huwezi kujua kuna kitu gani kilijitokeza hadi akapata maamuzi ya kuhama mkoa.
Usihukumu kwa haraka hivyo
Hakuna anayekatazwa kuhama iwe kwa hiari, ugomvi au ugumu wa maisha kama mzazi una wajibu wa kumtembelea mwanao japo mara 1 kwa mwaka ili kujenga uhusiano na mwanao, nimeshuhudia mama aliyekataliwa na mwanae baada ya kupoteana nae kwa miaka 35 naye aliachwa mtoto mdogo anayetambaa. Mama umeweza kumuhifadhi mwanao tumboni miezi 9 ulipo na mwanao yupo unamuachaje mwanao miaka mingi
 
Back
Top Bottom