Naungana na Msangafm kwa hilo.
Ila wakati mwingine kiswahili huwa tunapeana tu sikukuu njema, yenye heri na fanaka!
Hii inatokana na kuwa ki mila na utamaduni watanzania tulikuwa hatubaguani ki dini, hivyo basi zote zikawa sikukuu tu, yaani Noeli, Iddi, Pasaka, Maulid, za mashujaa au hata za huu uhuru mchwara tulosherehekea juzi! Sikukuu ya Noeli au Idi Majirani, ndugu, jamaa na marafiki bila kujali dini zao wanajumuika pamoja na kusherehekea pamoja.
Hii ni kama vile kiswahili hakuna "He" na "She" unapomzungumzia au kuelezea mtu (binadamu) kiswahili wote ni sawa na hakuna sababu unapomtaja mzazi, mwalimu, jirani, ndugu nk uelezee jinsia yake kwani havihusiani kabisa. Kama ni mwalimu ni mwalimu tu, mzani ni mzazi tu, meneja ni meneja tu, polisi ni polisi, jirani ni jirani tu nk. hashima haiongezeki au kupungua kwa sababu yeye ni wa kike au kiume! Sherehe za kidini ni vivyo hivyo! Sote tutasherehekea pamoja na majirani, ndugu na marafiki bila kujali wao wasalia msikitini, kanisani au wana dini zao za kale.