tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,854
- 1,129
Wana Jf habari zenu, kwanza natanguliza shukrani kwa wote wanaoleta na kuchangia mijadala yenye tija kwani imekuwa ikinijenga kila siku. Wadau nilikuwa na "Penpal friend" wa kike, toka nikiwa form.... na yeye alikuwa form...., nakumbuka alijieleza vilivyo jinsi kwao walivyo "familia bora" nami sikumficha nilimweleza ufukara uliokuwa ukiniandama, urafiki uliendelea na "automatically" tukawa wapenzi kipindi nipo A level. Nilifanikiwa kuonana naye nikiwa "first year" , "First time" naonana naye aliniita kwao, ukweli niliouona ni kwamba maisha yao ni bora sana ukilinganisha na ya kwetu/kwangu. Kikubwa nilichoki-note toka kwake ilikuwa ni jeuri na dharau ambavyo vilinichosha kadri siku zilivyokwenda, kuna kipindi alikuwa anadiriki hata kunifokea, ndipo niliposema ya nini malumbano? Niliamua kukaa pembeni, nakumbuka nilibadilisha mpaka namba kuepuka usumbufu wake. Sasa hivi majuzi kafanikiwa kupata namba, kanitafuta na tumeonana. Sera aliyokuja nayo ni kuniwezesha kupata kazi kupitia kwa ndugu zake. Kinachonitatiza ni ujeuri na dharau zake, hivi nikifanikiwa kupata kazi kwa juhudi zake haiwezi kuwa mtego wa kuninasa? Na nikipata alafu nikamkataa hawezi kuleta matatizo? Naomba mawazo yenu kwani ajira nahiitaji ila mapenzi na yeye siyataki!