Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 866
Nikiwa nimekaa nyumbani kwangu jana usiku nikifuatilia tamthlia ya Ruby mara nikapata mgeni.Mgeni huyu ni jirani yangu.Akaniomba nitoke nje ili tukaongelee huko.Akanileleza habari yake kwa kirefu.Kifupi ni kwamba yeye ni binti wa miaka 33 ana mtoto aliyemaliza darasa la saba mwaka jana na mtoto huyo amechaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza hapa jijini Dar es salaam.Anasema kwamba mtoto huyu baba yake alimkataa tangu akiwa mimba hovyo kwa kipindi cha miaka yote hii amekuwa akimtunza yeye mwenyewe.Yeye anafanya kazi za kubahatisha.Baada ya mtoto wake huyu kufaulu anahitaji mahitaji mbalimbali ya kumfanya aweze kwenda shule na yeye uwezo hana.Baada ya kutafakari kwa kina akaona bora amtafute mwanaume fulani aliyekuwa akimtongoza siku za nyuma kwa lengo la kuomba msaada wa fedha ili mwanae aende shule.Jamaa akampa masharti huyu dada kwamba kama anataka kumsadia ni lazima akubali afanye naye mapenzi.Mdada hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali..Anasema baada ya kufanya mapenzi na bwana huyu,bwana huyu akaingia mitini bila kumpa dada huyu ujira wake..Hivi sasa dada huyu ni mjamzito na jamaa hapokei kabisa simu za huyu dada..Dada huyu kanifuata jana na kutaka nimpe hela ili aende akatoe mimba kwani anadai hawezi kuzaa mtoto mwingine asiye na baba.Imani yangu ya dini hairuhusu kutoa mimba wala mimi mwenyewe kama mwanaharakati siungi mkono suala la kutoa mimba..Nimemkatalia kabisa,najua ujirani wetu uko mashakani..Niko njia panda.