Anataka tuachane na tayari nimekwishalipa mahari kwao na mipango ya ndoa ipo

Watu Huwa mnanichekesha sana nyie!

Unaishi ndoa pika pakua halafu una stress za kufunga ndoa!!

Yaani unafanya ndoa tayari halafu unawaza kufunga doa ambayo tayari unaiishi!!!

Wewe ungeendelea kumzalisha huku ukiona msimamo wake!unahofu ya nini!!?
Jamaa ni mazuu .... hayo tunaita matatizo ya mpumbavu ....ni sawa sawa na zile familia zinazo jali makaburi kuliko maendeleo...wapo tayari kutumia mamilioni kujengea makaburi wakati wao na watoto wao wanaishi kwenye mabanda ya kuku.
 
Achana naye usilazimishe huyo hakutaki endelea na mipango yako ya maisha
 
Hii imeendaa 😂😂😂 hao viumbe ni matapeli hawana mfano. Kikubwa we jua tu kuwa imeisha hio na huko aliko kwa bibi ni kwa mume mwenzio!
 
Kama wewe ni mtu WA kisasi,mpotezee kausha, tafuta mke mwngine, Wana wake wengi sana wanasaka ndoa, ila utakuja kulipa kisasi siku anafunga ndoa unaweka,kikwazo kuwa ni mchumba wako na mahali ulitoa, bint aolewi.

Pia kama sio mtu WA kisasi, samehe kila kitu kuanzia mahali ad mchumba huyu atakuja anasotea matako kuomba radhi umrudie alipitiwa na shetan
 
Mkuu pole sana! Kuna watu ni wakatiri sana aiseee…Mkuu achana nae kabisa kata mawasiliano naye na usikubali kabisa kusuluhishwa na mtu yeyote kabisa kamwe usikubali huyo mwanamke hakupendi na hakutaki kabisa!
Ila wanawake muda mwingine unaweza usiwaelewe kabisa unaweza kuta anadanganywa na kajamaa wala hakato muoa kabisa na akana mpango kabisa!

Kitakachofata hapo ni wewe kusumbuliwa na huyo binti na watu ili msuluhishwe..kamwe usikubali kuwa na suluhu na mtu aliyekukataaa kwenye hiyo hatua …..usikubali suluhu hiyo kamwe kamwe…tafuta mwanamke mwingine oa huyo achana nae kabisa wala usikubali kukaa kikao nae….
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…