Anatamani kurudi

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Hebu fikiria kwamba umefukuzwa kazi au kufilisika kimali, halafu mkeo au mpenzi wako anafanya visa na mikasa ya kila aina ili aweze kuachana na wewe. Hatimaye anafanikiwa na uhusiano wenu au ndoa yenu inavunjika.
Lakini miaka michache baadaye, Mungu siyo Athumani, unarudi kwenye ‘chati.’ Huyo mwanamke anapata taarifa huko aliko, na anaamua kujileta kwako, yaani kujipendekeza ili arudi. Hebu niambie, kama ni wewe ungefanya nini katika hili?
 
hapo ni sawasawa na kurudisha bomu ndani ya nyumba yako.
 


...akili kichwani! kiapo cha ".....kwa shida...." hau apply kwa mwenza wako huyo!
 
Huyo mke hafai kwani anakupenda muda wa raha tu ila muda wa dhiki/shida haonekani. Napata picha kama mume akija kuumwa na hajiwezi ataondoka pia ateseke peke yake akipona atarudi tena kujipendekeza!

Hata kanisani muda wa kiapo cha ndoa husema "nitakupenda kwenye raha na shida". Na mke atakuwa hakusema kutoka moyoni na ndio maana hatekelezi kwa vitendo sheria husika!
 
I, Bishanga Abashaija, do hereby take you Husninyo,as my lawful wife,and i promise to LOVE,CARE and CHERISH you ......until kifo kitutenganishe.....(best man TF)
Mkuu easily said than done ,hata sisi wanaume tunafanyaga mafyongo haya haya hasa mke anapougua kwa muda mrefu,wanaume kibao huwa wanajitia uwezo wa kuuguza umewaishia mke anaambiwa akaugulie kwao.....maisha haya bana we acha tu.
 
Akina baba mnavyotutelekeza na watoto? Mkiukwaa mnarudi tuwafunge nepi, mbona sie tunawapokea?
Anyway, ndivyo mlivyo tukikosea kidogo mnatunanga kama nini, kwani sie shetani huwa hatupitii?
Haya bwana
 
Nimeamini uzee una busara, asante kwa kuliona hilo.

 

Anarudi tu Nyumbani maisha yanaendelea kama kawaida.
 
Dah! Bishanga mbona hii ndoa umejihalalIshia fasta...lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…