Anatapika nyongo kila anaposwaki (kusafisha kinywa)

Izz

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
750
Reaction score
322
Kuna Dada mmoja ananiambia kila aamkapo asubuhi huwa anajisikia hovyo hovyo kwa kifupi ni vibaya yaani hawezi kuelezea hiyo hali.

Na kila anaposwaki (usafi wa kinywa) automatically atatapika nyongo ya rangi ya njano, na process nzima inampelekea machozi kutoka na kamasi jembamba.

Baada ya kutapika nyongo ndipo sasa ujisikia vizuri na ile hali ya hovyo hovyo uondoka na yenye kuchangamka muda wote. Ila jua linapozama ile hali ujirudia tena.

Je, hilo linaweza likawa tatizo gani? Yeye binafsi anahisi uenda akawa ni mjamzito, jumatatu ndio ana appointment ya kumuona daktari!

Haya JF Doctors tililikeni.....
 
Da. Pole mdau mie pia nilipatwa na hali iyo wakati ninamimba changa ingawa hata ilipokomaa Bado hali ilijirudia nilipokuwa na maralia
 
mpaka uende kwa dokta ndo ujue una mzigo?
kanunue rapid pregnancy test duka lolote la madawa,
buku tu,
kojolea
jibu hilo.
 
Wadau ahsanteni kwa kuja, yule demu lishakwenda hospital na kufanya vipimo vyote!.....Mrejesho ni kwamba tayari kitu kimejipa (ana mimba)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…