Anaweza kupokelewa shuleni mwakani?

Anaweza kupokelewa shuleni mwakani?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Ni kijana wa kiume aliyemaliza kidato cha nne mwaka Jana na kuchaguliwa kuendelea na kidato cha tano mchepuo wa Sanaa mwaka huu.

Hakuweza kuripoti shuleni mwaka huu kwa sababu alikuwa mgonjwa. Nduguze hawakutoa taarifa shuleni.

Anaweza kupokelewa tena shuleni endapo mwakani ataamua kwenda kuripoti?

Kuna anachoweza kufanya kwa sasa ili "kuiokoa" fursa yake ya kusoma?
 
Mpe pole kiukweli sijajua utaratibu ukoje ila kama wakimkatalia basi mpelekeni hata Chuo tu mbona hizi form 5&6 hazina maana yoyote kwasasa.
 
Ni kijana wa kiume aliyemaliza kidato cha nne mwaka Jana na kuchaguliwa kuendelea na kidato cha tano mchepuo wa Sanaa mwaka huu.

Hakuweza kuripoti shuleni mwaka huu kwa sababu alikuwa mgonjwa. Nduguze hawakutoa taarifa shuleni.

Anaweza kupokelewa tena shuleni endapo mwakani ataamua kwenda kuripoti?

Kuna anachoweza kufanya kwa sasa ili "kuiokoa" fursa yake ya kusoma?
Kwanza pole kiongozi kwa saibu hilo. Ninavyofahamu na pia ningependa ufanye yafuatayo:
1. Tafuta mawasiliano ya shule aliyochaguliwa kijana huyo upate ya mkuu wa shule na umweleze kinaga ubaga kuwa kijana alikuwa mgonjwa mwalimu atakuelewa sana na hapo atamuadimiti (apampa admission number) na kuweza kusomeka mwanafunzi alieripoti shuleni ama anaesoma kidato cha tano!!
2. Mwakani januari anaweza akaanza kidato cha tano kwa masomo ya sanaa anaweza akafaulu vizuri sana tu kikubwa ni mtoto kupambana zaidi na kujiamini kwamba anaweza akasoma bila shida
3. Kikubwa tafuta namba za mkuu wa shule aliyochaguliwa au makamu wa ake ikiwezekana hata muda huu
 
Back
Top Bottom