Anayeajiri na kufukuza makocha wa Taifa Stars ni nani ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Naomba kufahamishwa mwenye jukumu hili la kuajiri na kufukuza makocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania .

Je ni Wallace Karia ambaye ni Rais wa TFF au Katibu wake , ama ni kamati ya Utendaji ? na ni nani anayetoa wazo la mabadiliko hayo kwa maana ya Think Tank wa TFF ?

Kwa mfano , kikao cha kumuondoa Kim Poulsen kimefanyika wapi na wajumbe walioshiriki ni akina nani ?
 
Kwa mamlaka waliyopewa na Katiba ya TFF kama taasisi ya serikali. Sio kila waraka wa serikali unatakiwa wauone raia wasio watumishi wa umma
TFF ni taasisi ya Serikali ?
 
TFF ni taasisi ya kiserikali?????


TFF ni taasisi ya Serikali ?

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litalazimika kutafuta vyanzo vipya vya mapato yake ili kumlipa kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwassa baada ya Serikali kueleza kuwa hakuna ulazima wa kuendelea na utaratibu wa kuwalipa makocha wa timu za Taifa katika uongozi wa awamu ya tano.

Wakati wa utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliidhinisha Serikali kuwalipa makocha wa timu za Taifa za soka, riadha, judo, ngumi na netiboli, mchakato alioeleza kuwa ungeendelea katika vyama vingine, ingawa hadi anaondoka madarakani Oktoba mwaka huu ni vyama vitano pekee vilinufaika na mpango huo.

Ofa hiyo kwa vyama vya kitaifa ilikwenda sanjari na TFF kuwaleta nchini makocha Marcio Maximo, Jan Poulsen, Kim Poulsen, Mart Nooij na sasa timu hiyo inanolewa na mzawa, Mkwassa, lakini pia timu yao ya vijana iliwahi kunolewa na kocha Jacob Michelsen.

Mbali na soka, riadha ilinolewa na Andrea Curtius Baro, ngumi ilikuwa chini ya Pimentel Hurtado, Simone Mackiness aliletwa kuifundisha timu ya Taifa ya netiboli na Valdes Pepe kwenye judo na wote walikuwa wakilipwa na Serikali.

Hata hivyo, hadi Rais mstaafu Kikwete anaondoka madarakani, ni soka pekee ndiyo ilikuwa imebakia kwenye utaratibu wa makocha wake kulipiwa na Serikali na hata baada ya kuachana wa wageni, Serikali kupitia kwa katibu mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ambayo sasa ni Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel ilisisitiza kuendelea na mchakato wa kumlipa Mkwassa kama ilivyokuwa ikifanya kwa watangulizi wake, lakini kwa sharti la TFF kufuata taratibu.

Hata hivyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa ikilibana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulipa kodi kwenye mishahara ya makocha hao wa kigeni.


Uamuzi huo wa TRA umesababisha kuzuiwa kwa akaunti za shirikisho hilo kwa madai ya kutolipwa kwa kodi hizo za mishahara ya makocha.

Wakati hayo yakiendelea, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue aliliambia gazeti hili jana kuwa hakuna ulazima wa Serikali ya awamu ya tano kuendelea na utaratibu wa kuwalipa makocha wa timu za Taifa kama ilivyokuwa ikifanywa wakati wa uongozi wa awamu ya nne.

“Makocha wale waliletwa na rais mstaafu, lakini hakuna ulazima wa rais wa sasa (Dk John Magufuli) kuendelea na utaratibu huo,” alisema Balozi Sefue akifafanua kashfa ya ukwepaji kodi kwa makocha hao iliyosababisha TRA kuzuia fedha za TFF ili kufidia deni hilo.

“Suala la kodi za makocha hao hilo lipo chini ya Wizara ya Michezo, ndiyo inatambua masharti iliyopewa, kama walipewa msamaha wa kodi, pia waseme, hilo linawahusu wao kwani ndiyo walikuwa wakitekeleza mchakato mzima wa makocha hao na masharti waliyopewa wanatambua,” alisema Balozi Sefue.

Kwa upande wake, katibu mkuu wa wizara hiyo, Profesa Ole Gabriel alipoulizwa kuhusu masharti waliyopewa kwa makocha hao alisema alikuwa kwenye kikao, hivyo asingeweza kulifafanua suala hilo na kutaka apewe muda hadi Jumatatu.

Akizungumzia hatua hiyo, mkufunzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Henry Tandau alisema Serikali ipo sahihi kueleza hivyo, lakini iweke wazi ni nini kitafanyika kwa manufaa ya michezo kitaifa kwa ujumla.
 

Haya maneno chini umeyaelewa vizuri?

(((((Ofa hiyo kwa vyama vya kitaifa ilikwenda sanjari na TFF kuwaleta nchini makocha Marcio Maximo, Jan Poulsen, Kim Poulsen, Mart Nooij na sasa timu hiyo inanolewa na mzawa, Mkwassa, lakini pia timu yao ya vijana iliwahi kunolewa na kocha Jacob Michelsen.))))
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…