Anayeajiri na kufukuza makocha wa Taifa Stars ni nani ?

Unafahamu kuwa serikali hairuhusiwi kuingilia chochote cha tff? Zaidi ya kusaodia tu inapobidi?

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa jana ametoa maelekezo mazito kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) yanayolenga kuboresha mchezo wa mpira wa miguu nchini.

Maelekezo hayo ameyatoa katika mkutano wa Waandishi wa Habari aliofanya katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao na Viongozi wa TFF, BMT na watendaji wa Wizara. Amefafanua kuwa Serikali ipo katika mikakati kabambe ya kuboresha miundombinu ya michezo katika shule 56 nchini ikiwa ni pamoja na kufunga mashine za kisasa za kufuatilia michezo (VAR) kwenye viwanja vitano kwa kuanzia pamoja na kujenga vituo vikubwa vya michezo

Akitoa maelekezo ya Serikali, Mhe. Mchengerwa amesema BMT ikutane na TFF mara moja kujadili namna ya kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Sheria na taratibu za mchezo huo pendwa nchini ambapo pia amesisitiza kuwa Kamati inayohusika na Waamuzi ijitafakari kwa kuwa hadi sasa kwenye msimu huu wa ligi tayari imeshawaondoa waamuzi 13 kwa makosa ya upendeleo na rushwa.

Mhe.Mchengerwa amesema, TFF ikutane na waamuzi wote ili kupata uvumbuzi wa changamoto na sintofahamu zinazoendelea kujitokeza katika mchezo huo kinyume na sheria ambapo ameagiza TAKUKURU washirikishwe ili waweze kutoa elimu ya rushwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
Amefafanua kuwa, iwapo vitendo vya rushwa havitadhibitiwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu, mchezo huo hautakuwa na maendeleo.
 
Unafahamu kuwa serikali hairuhusiwi kuingilia chochote cha tff? Zaidi ya kusaodia tu inapobidi?

Serikali yakubali mipango ya TFF​

6 months ago
Serikali imeridhishwa na kuthamini hatua zinazochukuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ katika kujenga na kuboresha miundombinu rafiki ya Soka ili kuendelea kuibua na kuendeleza vipaji kwa vijana.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu ametembelea kujionea mradi wa ujenzi wa kituo cha michezo cha kisasa kinachojengwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa ufadhili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Yakubu ametembelea kituo hicho cha kitaifa cha mfano Februari 28, 2022 ili kujionea hatua zinazochukuliwa na TFF katika kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kujenga miundombimu ya mchezo nchini ikiwemo soka.

“Mradi huu ambao unatekelezwa na TFF kwa ufadhili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ni mkubwa, una ghorofa tatu ambazo zinauwezo wa kuchukua vijana 72 kwa wakati moja na katika eneo hili yatakuwepo maghorofa ya namna hiyo saba, haya ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya TFF na FIFA” amesema Naibu Katibu Mkuu Bw. Yakubu.
Katika kuhakikisha sekta ya michezo nchini inakua, Naibu Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema kuwa uendelezaji wa miundombinu ya michezo nchini ni kipaumbele cha Serikali ambapo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imejipanga kujenga viwanja 56 katika shule mbalimbali nchi nzima ambavyo lengo lake ni kulea vipaji vya vijana katika michezo.

Amesema Serikali inaendelea kuimarisha michezo nchini kwa kushirikiana na wandau mbalimbali ambapo imejipanga kuwa na kanda sita za vituo mahiri katika michezo nchini ambapo watashirikiana na wadau wa michezo ikiwemo TFF na wadau wengine ili kuhakikisha michezo yote inaendelezwa na kuibua vipaji vingi zaidi nchini.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema kuwa kituo hicho kitasaidia pia kutoa mafunzo kwa walimu na waamuzi wa soka watapata fursa ya kufundishwa ili kuondokana na malalamiko yanayotolewa na wadau wa michezo pamoja na mashabiki wa soka nchini.
Kwa pande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bw. Wallesi Karia ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wanaopata ikiwemo kutembelea mradi huo kujione hatua waliyofikia ili kutimiza ndoto ya shirikisho hilo ya kuwa na vituo vya mfano ambavyo kwa sasa vinajengwa vituo viwili, kimoja kinajengwa Kigamboni jijini Dar es salaam na cha pili kinajengwa mkoani Tanga.

“Mradi wetu kwa eneo ya majengo tayari umekamilika kwa asilimia kubwa, kwa upande wa viwanja bado ujenzi unaendelea, kiwanja cha nyasi bandia kipo tayari bado kubandika nyasi ambazo nazo tayari zipo hapa, lakini kwa upande wa kiwanja cha nyasi za kawaida tunatarajia zitapandwa mwezi huu wa tatu ambazo zitatakaa kwa muda wa siku 40 na baadaye zitakatwa ili kusawazisha na kuanza kutumika” amesema Bw. Karia.
Rais huyo wa TFF amesema Shirikisho hilo linatarajia kukabidhiwa mradi huo wa awamu ya kwanza ifikapo mwezi Juni 2022 ili kuruhusu awamu ya pili ya ujenzi wa viwanja vingine hatua itakayoongeza wigo wa vijana wengi kupata mahali pa kufanyia mazoezi kwenye viwanja vyenye hadhi ya kimataifa.
 
Noma sana !
 
Hata hawa makocha wapya akiwemo Kaseja ni nani aliwapendekeza ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…