Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Kama una akili timamu na unawaza kwa kutumia kichwa na sio tumbo (maslahi binafsi) utagundua kuwa Nchi yetu imefika hatua mbaya sana.
Kiongozi yeyote anapojua kuwa sio kura za Wananchi zinazoniweka Madarakani kamwe hawezi kuogopa kuwaibia hao wananchi fedha zao (kodi zao)
Kiongozi yeyote anapojua kuwa sio kura za wananchi zinazoniweka madarakani hawezi kuogopa kupiga madili kwa faida zake na familia yake kwa sababu kamwe wananchi hamuwezi kumfanya chochote.
Kiongozi yeyote anapojua kuwa sio kura za Wananchi zinazoniweka madarakani hawezi umiza kichwa chake na kuhangaika kuhakikisha matatizo ya Wananchi husika yanapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Hii ni kwa sababu sio hao wananchi wanaoamua awe kiongozi.
Pamoja na nchi yetu kuwa na rasilimali nyingi, hadi leo ina umasikini wa kutisha kwa wananchi wake.
Maeneo mengi nchi hii Barabara ni mbovu na hata zile ambazo zimejengwa zinajengwa kwa kiwango duni.
Maeneo mengi nchi hii hayana huduma bora za afya na hata yale yenye huduma hizo, huduma husika zinapatikana kwa shida. Utakuta hospitali haina vifaa, haina wataalam au haina madawa ya kutosha.
Maeneo mengi nchi hii hayana hata huduma bora za kuzoa takataka. Suala dogo la Kudhibiti taka limegeuka kuwa suala kubwa. Hakuna magari ya kuzoa taka yanayozoa kila siku, hakuna mfumo mzuri wa kudhibiti taka masuala ambayo ni ya kawaida sana.
Leo hii elimu wa watoto wetu ni kizungumkuti. mtoto kusoma shule ya Serikali ni kama unampeleka mwanao akawe mjinga. Hakuna maarifa sahihi wanayopata watoto wetu kwenye shuule hizo yanayoweza kuwafanya wawe na soko kubwa kwenye dunia hii ya ushindani.
Maeneo mengi ya nchi yetu hayana maji ya uhakika pamoja na nchi yetu kuzungukwa na maziwa makubwa matatu na Bahari ya Hindi. Wananchi wengi hawana maji safi na salama kwa matumizi yao. Hata wale wenye hayo maji wanayapata kwa mgao hadi limekuwa jambo la kawaida sana.
Leo hii masuala ya kawaida sana kama ujenzi wa mpangilio unaozingatia mipango miji inaonekana ni kama suala la anasa wakati kiuhalisia kila mwananchi wa nchi hii anapaswa kuishi kwenye maeneo safi yaliyopangiliwa vizuri.
Matumizi mabaya ya kodi za wananchi nalo limekuwa jambo la kawaida ambapo tunaona Viongozi wa kisiasa wakiongeza gharama za miradi ili kuiba fedha za Wananchi. Wanatumia fedha za wananchi kama wanavyopenda kwa masuala ambayo hata hayajawahi kuidhinishwa na Bunge ambacho ndo chombo kinachopaswa kusimamia na kuidhinisha matumizi ya fedha za wananchi.
Kwa Watanzania wanaodhani masuala haya yanatokea kwa bahati mbaya, wanakosea sana. Msingi mkuu wa masuala haya ni kutoheshimika kwa kura ya mwananchi. Viongozi wanatambua sio mwananchi anayewaweka na kuwatoa madarakani ndo mana leo hii tunaona kila kitu hakiendi sawa.
Agenda ya CHADEMA ina nia ya kurekebisha haya masuala. Kuna watu wanadhani endapo mabadiliko haya yakifanyika wanaonufaika ni CHADEMA. La hasha wanakosea sana.
Endapo nchi hii leo itaweka mfumo wa haki unaosimamiwa vizuri wa Uchaguzi utakaofanya kura ya Mwananchi wa kawaida kutoibwa, kuhesabiwa na kuhesabika faida ni kwa sisi Wananchi ambao tutakuwa na mamlaka na Viongozi wetu hivyo Viongozi watalazimika kufanya mambo kwa faida yetu.
Viongozi wakiona Wananchi tuna mamlaka dhidi yao kupitia sanduku la kura, kwa utajiri wa Rasilimali tuliokuwa nazo Tanzania, watoto wetu watasoma kwenye shule bora, tutatibiwa kwenye hospitali bora zenye vifaa bora na huduma bora, hatutakosa huduma muhimu kama maji na umeme maana fedha zitawekezwa kujenga na kutunza miundominu ya maji na umeme na kuhakikisha maji yapo kwenye kila nyumba tunayoishi, takataka zitazolewa mitaani kwetu wakati wote na mitaa yetu kuwa misafi wakati wote, na mwisho tutaishi kwenye makazi bora na kutembea kwenye miundombinu bora ya barabara zilizojengwa vizuri na zinazotunzwa vizuri hadi kwenye mageti ya nyumba zetu.
Ombi langu, kwa yeyote anayedhani No Reform No Election ni kwa faida ya CHADEMA atumie kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ranadhani pamoja na kwaresma inayoanza kesho kutubu kweli.
Kwa wale wasioamini kwenye Mungu, tumieni kipindi hiki kutafakari na kutumia your consciousness kubadili hiyo misimamo yenu na kuamua kuunga mkono jambo hili ambalo kimsingi ndilo litakalolikomboa Taifa letu.
Lord denning
Mtanzania Mzalendo