Anayefahamu ugonjwa huu wa ngozi,Streptococcal Necrotizing Fasciitis

Anayefahamu ugonjwa huu wa ngozi,Streptococcal Necrotizing Fasciitis

Malungwana

Senior Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
187
Reaction score
99
Streptococcal Necrotizing Fasciitis

Ndugu wana jamvi, mwenye ufahamu na ugomjwa huu hapo juu naomba anifahamishe matibabu yake, kuna ndugu yangu nimembiwa ana ugonjwa huu, alianza kutoka kama malengelenge kwenye mkono karibia na bega, yakipasuka yanatoka maji , yale maji yanapofika yantoa malengelenge mengine kwenye mkono, unashambualia ngozi haraka sana, akanza kua kama aliyeungua moto, baada ya siku mbili tu hali ikawa ni mbaya zaidi,kafanya vipimo vyote vya damu, yuko salama, nime attach picha, hii hali ni siku ya pili ndio alikua hivyo, alikwenda hospital ndio Doctor akasema ni ugonjwa huo, unasababishwa na bacteria ambao wanashambulia nyama za mwili haraka sana, amepata matibabu kwa kiasi anaendelea vizuri, ila haponi kwa haraka sana.

Naomba mwenye maelekezo na ushauri zaidi,

Naomba kuwasilisha.
 

Attachments

  • IMG-20170801-WA0004[1].jpg
    IMG-20170801-WA0004[1].jpg
    102.3 KB · Views: 53
  • IMG-20170801-WA0005[1].jpg
    IMG-20170801-WA0005[1].jpg
    77.2 KB · Views: 58
Dah A deal na wataalam wa afya msije kushawishika ku deal na wapiga ramli!
Mpe pole dada yetu dua zetu zinaelekezwa kwake pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee mpe pole sana!

Necrotizing fasciitis ni mkali sana hutokea haraka na usambaa kwa haraka sana.
Dalili zake huwa ni homa,rangi nyekundu au zambarau ktk sehemu iliyoathirika,maumivu makali na pia kutapika.
Ugonjwa huu mara nyingi hutokea miguuni,mikononi na sehemu ya siri .
Ugonjwa huu huingia mwilini kupitia sehemu ya ngozi iliyochanika au kuungua moto.

Watu walio ktk hatari ya kupata ugonjwa huu ni walio na kinga ya mwili isiyofanya kazi vizuri kama kisukari au saratani,wenye uzito mkubwa,walevi wa pombe,matumizi ya dawa kupitia mishipa ya damu.

Matibabu yake:-
.Usafi wa hali ya juu wa sehemu iliyoathirika pamoja na mikono
.Kuondoa sehemu ya ngozi iliyoathirika (surgical remove),hii hufanywa na madaktari
.Antibiotics, mara nyingi hutolewa kwa combination. Ni vyema kufanya uchunguzi wa bacteria aliyesababisha ugonjwa ili kupata mafanikio bora ya dawa iliyochaguliwa/zilizochaguliwa
.Wakati mwingine kukata kabisa mguu au mkono hufanyika(Mwenyenz Mungu amuepushe)

.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom