Anayeifahamu COASCO.... taarifa zake please.

Kaka mimi siwajui vizuri ila kwa mtu wa ngazi unayoitiwa ni Coas 4 - Tshs 769,241 kwa mwezi. suala la malulupu inategemea sana. Ingawa walikuwa na mze mmoja wakichaga ambaye ameharibu saana shirika hilo maana kwa sasa perfomance yao ni chini ya aslimia 50%. Uchaguzi ni wako.
kaka coasco ni shirikisho la ukaguzi la vyama vya ushirika,kazi yao ni kukagua vyama vya ushirika,sina uhakika na malipo yao ila kuna maslahi mazuri,nishafanya nao kazi walikuja kukagua vyama vyetu,mie ni afisa ushirika.
 
Kama nilivyo sema hapo mwanzo Ni tshs 769,241..
 
Kwa hili hata kama ni ukweli halina uhakika pamoja na shirika kujaa wachaga wote wanavyeti...... Ambao unasema hawana vyeti niwazee walioajiriwa na mfumo wa mwalimu Nyerere mtu ame maliza form iv apate ajira. Lakini kwa ajira ambazo mimi mwenyewe nilishiriki moja ya interview wote waliopata ajira ni gradute sasa sijui wewe unamaanisha kada ipi ambayo wameajiri pasi vigezo.

Hakuna mtu ambaye hana cheti na takukuru wamethibitisha hilo wasio na vyeti wote wamebakiza siku chache kustaafu. Naamini pia wako katika sekta nyingi za Tanganyika ndiyo maana ya madudu yanayoendelea.
wameajiri watu hawana hata vyeti kisa ni ndugu na dg au dhra.
 
lutamyo unachosema ni kweli kwa 85% ila tu COASCO watamkagua nani kwani Vyama vya ushirika siku hizi havipo na SACCOS zote zimeliwa na viongozi wao sasa hata ukikagua huna Mamlaka ya kuwashtaki wabadhirifu mpaka Mkutano Mkuu wa Mahesabu wa wanachama wote, kwa hiyo Money Maker km unataka uende ukatengeneze posho na Night ni ngumu jamaa yangu, hapo ni mpaka upangiwe Chama cha kukagua na huko Meneja/Mhasibu au Mweka Hazina awasiliane na Mwenyekiti wa chama wajadiliane ili wachomoe posho za wajumbe wakutupie ya lunch
Mshahara sio mbaya ila hutakuwa hapo Makao makuu Dodoma lazima utapangiwa kwenye Branch zao za Iringa, Arusha, na mikoani ombea upangiwe ile Mikoa yenye Ushirika hasa km Kagera, Kilimanjaro Mwanza, Mbeya Shinyanga, Arusha nk
La sivyo endelea hapo ulipo usije ukakosa kote maana hawa Maafisa Ushirika wa Hizo wilaya au Mikoa wana Conflict interest na usimamizi hasa suala la nani asikilizwe kati yao na Ma-Auditor wa COASCO
 

Maisha dodoma yako juu sana kwa sasa, kuanzia nyumba, chakula hadi bidhaa nyingine za dukani kama nguo.
 
Du unayosema ni kweli lakini yote hayo yalitokana na Mangi mmoja ambaye na sikia kasimamishwa kwa sasa yeye alipunguza ufanisi wa shirika katika ukaguzi zaidili lipaform vibaya. Ila sikubaliani na wewe kwa jambo moja SACCOS zilizosajiliwa ni zaidi ya 10000 ila zinazo perfom ni zaid ya 5000. Kwa sababu uongozi wa Mosha umeondoka tunaamini kuwa fedha tunazotuma hapo zitafanya kazi kwa sasa. Pia tambua kuwa afisa ushirika yeye ni kama internal auditor tena wengi wamesoma Mabnagement ya Ushirika na siyo wahasibu percer.
Na Mrajis ameahidi kuvirudisha vyama vyote vina vyokaguliwa na wakaguzi wengine ambao kwa kweli hawajui kitu hasa juu ya hali ya Ushirika nchini... Umesema vyama hamna kwa taarifa yako Mtwala tu ina kazi nyimbi tu, Dar pia na pwani na tanga kwa hiyo hata kama unachukia COASCO LAKINI SIYO KWELI UNAYO PUBLISH. NA SI KWELI KUWA JAMAA WANATEGEMEA POSHO ZA WAJUMBE WA BODI HAWA JAMAA WANAPEWA NIGHTOUT NA EXTRADUTY PIA HILO SIJALIBAINI.
 
kama ukipata nakushauri ufanye iyo kazi japo mshahara unaeza usiwe mkubwa at start,but with experience and certification,the accounting profession is one of the most rewarding despite the challenges
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…