Anayeifahamu hospitali ya Wilaya Morogoro Vijijini

Anayeifahamu hospitali ya Wilaya Morogoro Vijijini

Realbest

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2013
Posts
812
Reaction score
300
Habari za humu wakuu? Hivi kuna mtu anayeifahamu hospitali ya wilaya ya Morogoro Vijijini na mazingira yake Kwa ujumla? Kuna mdogo wangu kapangiwa kituo cha kazi huko .

Napenda kujua jiografia yake Kwa ujumla pamoja na wilaya ilipo. Pamoja na changamoto zake Kwa ujumla.
 
Ipo Morogoro vijijini, kwa akina babutale huko hamna network mpaka uende kwenye mti pana makopo yaliyo tundikwa uiweke simu yako hapo ukipigiwa boda boda watakuita.

Ila nikushauri nenda kafanye kazi maana maisha ni magumu ukiacha utajuta hakika utajuta naomba niishie hapo.
 
Vijiji vya siku hiz avina shida kwakua vingi vinauduma nyingi za kijamii....

Moro rural sijui kama pale makao makuu wamejenga hospital ila hosputal ilikua Duthumi....

Mvuha na Duthumi mazingira ni mazuri kwa biashara na kilimo pia..usafiri,umeme wa uhakika.
 
Njia unayopitia kutoka morogoro mjini je!?
 
Babu Tale njoo umpe jibu ndugu wa mpiga kura wako mpya wa mwaka 2025!

Inabidi uzitafute kura angalau ufikishe 20% za ndiyo za kura zitazopigwa sababu uwezo mdogo
 
Ipo Mvuha,usafiri kwa njia ya treni zaTazara unafika,na hata kwa barabara haswa hiki kiangazi ni uhakika,ni pazuri,maisha rahisi,biashara ya kilimo haswa mpunga na mbogamboga na matunda ndo penye
Aisee! Viwanja vyake vitakuwa Kisaki, Dutumi, Mngazi, Kangazi nk.

Joto la Kisaki limepungua na Mbu wa Kisaki wamepungua?
 
Habari za humu wakuu? Hivi kuna mtu anayeifahamu hospitali ya wilaya ya Morogoro Vijijini na mazingira yake Kwa ujumla? Kuna mdogo wangu kapangiwa kituo cha kazi huko .

Napenda kujua jiografia yake Kwa ujumla pamoja na wilaya ilipo. Pamoja na changamoto zake Kwa ujumla.
Ipo Mvuha, unashuka morogoro msamvu stand anapanda gari za kwenda kisaki anashukia mvuha.. nauli toka msamvu stand mpaka mvuha ni shilingi elfu 7.

Hospital iko palepale mvuha centre. Mazingira si mabaya sana
 
Yupo karibu na bwawa linalo jengwa la stigler, yupo karibu na hifadhi ya taifa ya nyerere...

Zamani ofisi za halmashauri zilikuwa mjini morogoro manspaa, ila baada ya Mh. Hayati kutaka kila halmashauri ziende ktk maeneo yao ndipo nao waka jisogeza huo

Ni halmashauri inayo pakana na mkoa wa pwani upnde mashariki kwa wilaya za kibaha, chalinze, kisarawe, kibiti na rufiji kama sija kosea

Sirjeff/Ontario nazani aliwahi kuandika kuwa ana mashamba ya mpunga huko Dutumi, kisaki...

Mikese (mizani morogoro) ni moja ya eneo ktk halmashauri ya Moro vijijini...
 
Habari za humu wakuu? Hivi kuna mtu anayeifahamu hospitali ya wilaya ya Morogoro Vijijini na mazingira yake Kwa ujumla? Kuna mdogo wangu kapangiwa kituo cha kazi huko .

Napenda kujua jiografia yake Kwa ujumla pamoja na wilaya ilipo. Pamoja na changamoto zake Kwa ujumla.
aende kwanza. hizo changamoto atazijua huko huko
 
Back
Top Bottom