Anayeifahamu Icheja wilayani Kwimba naomba anijuze machache

Anayeifahamu Icheja wilayani Kwimba naomba anijuze machache

kikoozi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2015
Posts
2,094
Reaction score
3,108
Ndugu zangu habari za muda huu, naomba kujuzwa kwa mabaye nafahamu MKOA wa MWANZA Halmashauri ya wilaya KWIMBA sehemu inaitwa ICHEJA.

Hali ya hewa ya maeneo hayo ipoje?
Ni umbali gani kufika mwanza mjini (jiji)?
Je, ni mbele ya mwanza jiji au ni nyuma ya mwanza jiji au ipo pembeni mwa mwanza jiji ?
Ustaarabu wa wakazi wa maeno ayo upoje?
shughuli za kiuchumi kwa ameno ayo ni zipi aswa?

Na mengineyo unayo fahamu kuhusu wilaya iyo ya KWIMBA

Je, unanishauri nini mimi ambaye nataka kutoka mkoa wa DAR ES SALAAM na kuamia WILAYA iyo

Karibuni kwa majibu na ushauri wenu.
 
Wananzengo miyeyusho pande hizo uwe nao makini, la sivyo utajikuta unachezea viboko.
 
nashukuru ndugu zangu, ila bado sijajibiwa maswali yangu kama nilivyo ulizwa ndugu zangu
 
Icheja ziko mbili mkuu kuna ile ilipojengwa halmashaur mpya na hospital ya wilaya na kuna nyingine iko vijijini uko ndani hatari
 
Mkuu kafanye kazi,kuwa na adabu ,huo ukanda ni walozi sana,wanamambo ya utamaduni.epuka ndoa za watu,don't talk much,fuata taratibu zao za kijamii Hasa kuhusu misiba kuchangia na kushiriki mambo ya msingi.usikubali wakujue sana,ukienda eneo jipya unatakiwa kuwa mkimya mkimya hata kwa miezi kadhaa ili ufahamu ni nani anaweza kuwa rafiki yako kulingana na itikadi zako ,don't trust people easily.
 
Nakushauri ujiandae kupambana ki kweli kweli watu wa huko wapo wa zama za mawe,za kati na za kisasa kidooogooo.

Ipo mbali na Mwanza jiji nauli toka huko mpaka jijini ni kuanzia elfu 7000 etc

Vitu bei kubwa kiasi

Jiandae kubanwa na masuala ya nzengo

Majungu kazini jambo la kawaida ila huko yamezidi
 
Kama sijakosea Icheja ipo Wilaya ya Kwimba takribani Km 35 kutoka Ngudu ambapo ndio makao makuu ya wilaya ya Kwimba. Pia ni kama Km 80 Kutoka Mwanza mjini. Icheja ni kijiji kilicho mpakani mwa wilaya ya Magu na Kwimba. Ni karibu kwenda Magu kuliko Kwenda Kwimba.

Hali ya hewa
Kwa ujumla hali ya hewa ni kawaida sio joto au baridi sana.
Tegemea kula mihogo na viazi sana pande hizo while ugali ni constant.
Shughuli kubwa ni kilimo cha mahindi, mihogo, viazi, pamba ,mpunga na ufugaji.
Maisha ni cheap ila kijijini sana
Wenyeji wanaongea kisukuma sana

Ushauri
Ukifika huko usijitenge sana na jamii changamana na watu utaishi vizuri sana.
Kama ni mtumishi na hujao ukifika tafuta nurse au Mwalimu maana vijijini pisi zinaolewa mapema labda ukutane na wanaosoma chuo.
 
Ipo Pembeni Ya Barabara Kuu Shinyanga ~Mwanza
Hali Ya Hewa Siyo Haba, Pale Mjini Bado Sana Pamepoa
Nenda Mkuu Kafanye Kazi Huko Wenyewe Wanasema Michele Tele
 
Baba yangu mdogo alihamia uko mpaka akafikia hatua ya kuhama serikalini kwenda private sector. Wachawi, wafitini, roho mbaya na hawapendi wageni. Ukiwa mgeni ukapanda cheo kazi unayo, wanataka wakukwamishe.
 
Karibu
Icheja ni kijiji dani ya kata ya bugandando
N karbia km30 kutoka wilayan kwimba au maarufu Ngudu
Wenyeji n wasukuma watupu na n kijijini kwa asilimia 100
Kwenda mwanza n rahisi kwa kupitia njia ya magu au njia ya sumve
 
shukrani sana mkuu, uniongezea jambo
 
Ipo Pembeni Ya Barabara Kuu Shinyanga ~Mwanza
Hali Ya Hewa Siyo Haba, Pale Mjini Bado Sana Pamepoa
Nenda Mkuu Kafanye Kazi Huko Wenyewe Wanasema Michele Tele
shukrani sana mkuu
 
Kama sijakosea Icheja ipo Wilaya ya Kwimba takribani Km 35 kutoka Ngudu ambapo ndio makao makuu ya wilaya ya Kwimba. Pia ni kama Km 80 Kutoka Mwanza mjini. Icheja ni kijiji kilicho mpakani mwa wilaya ya Magu na Kwimba. Ni karibu kwenda Magu kuliko Kwenda Kwimba.

Hali ya hewa
Kwa ujumla hali ya hewa ni kawaida sio joto au baridi sana.
Tegemea kula mihogo na viazi sana pande hizo while ugali ni constant.
Shughuli kubwa ni kilimo cha mahindi, mihogo, viazi, pamba ,mpunga na ufugaji.
Maisha ni cheap ila kijijini sana
Wenyeji wanaongea kisukuma sana

Ushauri
Ukifika huko usijitenge sana na jamii changamana na watu utaishi vizuri sana.
Kama ni mtumishi na hujao ukifika tafuta nurse au Mwalimu maana vijijini pisi zinaolewa mapema labda ukutane na wanaosoma chuo.
ubarikiwe sana sana sana mkuu, umenipa mwanga mkubwa sana
 
Karibu Kijiji Cha Nyamigamba Icheja, wilaya ya Kwimba mkoa was Mwanza, ni rahisi sana kufikika kama utapitia Magu ukiwa unatokea Mwanza. Ukifika Magu panda gari za kwenda Nyambiti, shukia Mwalinha, chukua bodaboda zikupeleke Icheja kwa Raha zako.
Wenyeji wake ni wasukuma 99%
Shughuli kuu ni kilimo na ufugaji,
Hali ya hewa ni ya kawaida, siyo joto Wala baridi.
 
Dah! Ila Tanganyika ni kubwa aisee! Imagine kuna maeneo wakazi wake mpaka leo wanatumia zaidi lugha zao za asili kuwasiliana, kuliko Kiswahili.
 
Back
Top Bottom