Kama sijakosea Icheja ipo Wilaya ya Kwimba takribani Km 35 kutoka Ngudu ambapo ndio makao makuu ya wilaya ya Kwimba. Pia ni kama Km 80 Kutoka Mwanza mjini. Icheja ni kijiji kilicho mpakani mwa wilaya ya Magu na Kwimba. Ni karibu kwenda Magu kuliko Kwenda Kwimba.
Hali ya hewa
Kwa ujumla hali ya hewa ni kawaida sio joto au baridi sana.
Tegemea kula mihogo na viazi sana pande hizo while ugali ni constant.
Shughuli kubwa ni kilimo cha mahindi, mihogo, viazi, pamba ,mpunga na ufugaji.
Maisha ni cheap ila kijijini sana
Wenyeji wanaongea kisukuma sana
Ushauri
Ukifika huko usijitenge sana na jamii changamana na watu utaishi vizuri sana.
Kama ni mtumishi na hujao ukifika tafuta nurse au Mwalimu maana vijijini pisi zinaolewa mapema labda ukutane na wanaosoma chuo.