kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
MTAALAMU wa tabia za wanyama aliyeamua kuishi na simba wawili kwa kipindi cha mwezi mmoja, ametimiza siku ya tano na tatizo lake kubwa ni kuchaniwa nguo. Jim Jablon anayeishi na simba ndani ya banda moja kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia chakula na matunzo kwa wanyama waliojeruhiwa porini, ameanza kuonja shubiri ya simba hao ambao katika siku tano tayari wamemchania suruali sita aina ya jinzi. Mtaalamu huyo anaishi na simba hao aliowapa majina ya Lea na Ed, kwa kipindi chote cha mwezi huu wa Januari, ambapo hata hivyo ndani ya banda hilo kuna sehemu za usalama kama simba hao watakuwa wakali kwake.
Jablon (42) ambaye anajiita mfalme wa porini alisema meno ya simba hao yamekuwa yakirarua suruali ambapo hadi sasa amelazimika kutupa suruali sita, kwakuwa hazivaliki tena. Alisema simba hao huwa wanakula mlo mmoja kwa siku, hali ambayo imemfanya na yeye awe anakula mlo mmoja kwa siku. Jablon anasaidiwa na binti yake Chelsey mwenye umri wa miaka 13 ambaye kazi yake ni kupeleka chakula na mahitaji mengine.
Jablon alisema chakula chake huwa anakula kwa kujificha ndani ya moja la banda lake la usalama aliloliweka juu ya mti.
Alisema yeye huwa anakula chakula kilichopikwa kwa kupelekwa na kuwekwa sehemu maalumu, ambapo simba hao hupewa nyama.
Jablon alisema wakati wa usiku huwa analala ndani ya banda lake la usalama alilojenga juu ya mti, urefu wa futi 12 kutoka ardhini, na kwamba eneo hilo simba hao hawezi kulifikia.
Alisema kwa ujumla simba hao huwa wanalaa kwa kati ya saa 18 hadi 20 kwa siku, ambapo na yeye hutumia muda huo kupumzika.
Jablon alisema pia ana eneo lingine dogo lenye uzio ambalo nalo ni kwa ajili ya usalama wake, kama simba hao watageuka mbogo kwake.