Anayejua mapishi ya makopa ya mihogo

Anayejua mapishi ya makopa ya mihogo

Candy kisses

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
297
Reaction score
210
Habari wanajamvi!

Naombeni mnielekeze mapishi ya mihogo ilokauswa (makopa). Nakumbuka nilishawahi kula hiki chakula nikiwa mdogo ni kitamu sana na nitamani nipike tena.

Nitashukuru sana kwa kuelekezwa pishi hili.

Wadigo wenzangu, Wabondei, Wasambaa naombeni uzoefu.
 
Kwanza kabsa kama unayo makopa yenyewe (yani mihogo ambayo ishaanikwa juani mpaka kubadilika rangi), Unachotakiwa kufanya roweka hayo makopa katika maji kama kwa siku moja si uanjua yanakuwaga magumu kama vigogo, kwahiyo yaroweke kwa usiku mmoja, halafu ndo usuueze yale maji ulorowekea ufanye kama unaosha kidogo unayabandika na kuipika kama mihogo ya nazi, ila makopa watia hiliki na sukari, Kama huna makopa una mihogo mizuri kwanza ianike juani mpaka ioze flani lol, baada ya kumaliza kuelezea nimeyatamani.
 
Unanitoa mate jamaniii...
 
Habari wanajamvi!

Naombeni mnielekeze mapishi ya mihogo ilokauswa (makopa). Nakumbuka nilishawahi kula hiki chakula nikiwa mdogo ni kitamu sana na nitamani nipike tena.

Nitashukuru sana kwa kuelekezwa pishi hili.

Wadigo wenzangu, Wabondei, Wasambaa naombeni uzoefu.

Njia mojawapo: Andaa makopa kwa kuyapaa, na uyapike kwa nazi, kwa kuwa yamekauka ni magumu yachemshe kwa muda hadi yalainike kiisha yaunge kwa nazi kama vile unavyopika mchele wa nazi na hata mihogo, magimbi nk
 
kwetu tunakula na karanga za chumvi hatuweki nazi,,,,nimeyamisi yaan
 
Back
Top Bottom