Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
"mungu mdogo" - hahitaji sheria,katiba,bunge bajeti wala ushauri wa shetani au malaika kufanya atakalo ,kwani jeshi na polisi si wanafuta amri yake?
(M)ungu na sio (m)ungu


Swissme
 
Kwamba unataka Tanzania iwe Rwanda? Mambo ya Rwanda yanaingia hapa kweli? Hakuna shaka yoyote wewe ndiye uko brain washed! Soma historia ya Rwanda na umsome Kagame mwenyewe, kisha uje kwenye historia yetu na umsome JPM...
 
Hivi ule utaratibu wa kupeana taarifa za mapato ya kila mwezi ziliishia wapi? Au tatizo ni nini?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Kahabaaa!!!
 
huu uzi tangu niuone just for the first time sikuwa na papara ya kutoa maoni kwa kumjibu mtoa hoja. BINAFSI MPAKA SASA NAONA MKUU ANATUPELEKA ANAKOJUA YEYE
 
Hivii makusanyo ya kodi TRA MWEZI ULEEE.. ULIOPITA... NA HUU SASA TUMEKUSANYA NGAPI VILEEE?[emoji84]
 
Ni vizuri tukajifunza katika Biblia jinsi tawala mbalimbali zenye nguvu zilivyaanguka kama nyumba ya mabua.

Tukisoma katika kitabu cha Danieli 5:1-10 Mfalme Belshaza wa Babylon alikuwa na nguvu na kiburi kingi sana katika utawala wake, wala hakutaka kushauriwa wala kukosolewa. Alijihisi yeye ndio anayejua kuliko watu wake wote, na mwenye akili nyingi kuliko raia wote. Hakutaka kushauriwa na yeyote hata wakuu wengine katika utawala wake waliiga matendo yake. Ila siku moja aliandaa karamu kuwafurahisha watumishi ndani ya utawala wake, ndipo Mungu alionyesha maajabu yake kiganja cha mkono kuandika juu ya ukuta Menemene=ufalme wako umepimwa=Peresi=umepungua au unamapungufu=Tekeli= umegawanywa nao umepewa wengine.

Utawala huu umefanania sana ufalme wa Babeli ambao Mfalme Belshaza alifikiri kuwa yeye anajua kuliko watu wote.

Utawala huu unahisi kwamba watu wengine hawafai kabisa kutoa mawazo yao maana ni ya kipuuzi.

Utawala huu unaongozwa na hisia na visasi, kuliko uhalisia. Utawala huu unafikiri kwamba watafanikiwa kuwafumba kinywa wote wanao wakosoa na kujaribu kuwashauri.

Utawala huu unapenda sifa na kujiinua. ni utawala unaotaka kuchukuwa utukufu hata wa Mungu.

Utawala huu umejaa watu wanafiki wasiokuwa na uhuru wa fikra bali wana nidhamu za woga.
kwa hali hii utaporomoka maana Mungu hawezi kuruhu watu kunyimwa uhuru wa kutoa hisia zao.
 
Unabii huu hatari,Mungu ni Mwema tutajua......anguko la karne
 
Naona utawala huu "utafitinika' na kila asiye amini NENO atashangaa.....
 
tanzania hii sio ile ya miaka iliyopita,huu si muda wa maneno ,ni wkt wa vitendo,chama tawala kutafuta kick ni kupoteza muda,maisha mtaani ni magumu both kwa wapiga dili na wasiopiga,raia tunaumia kuliko viongozi,wao hawajali kuhusu ugumu wa maisha,ni kutafuta kick,mala makanikia ,kama escrow,mara kibiti,mara fly over,mala train ya umeme,mi wakijini vinanisaidia nin wkt barabara vumbi,umeme hakuna,maji shida,zimejaa dispensar zisizo na dawa,tunafanya kz kwa bidii lkn pesa imekuwa ngumu,nimemkumbuka san nyerere,baba popote ulipo maisha ni magumu,matukio ya kujinyonga yameongezeka kwa sabab ya maisha,wanaume hawaoi sasa,tunafursa moja tu ya kujikomboa nayo ni 2020,tufanye maamuzi magumu jaman .mtazamo wangu tu
 
Ukiona Baba akiulizwa swali anakuwa mkali ujue hana jibu,
Hajui akujibu nini,
Hajui anakifanya kitamfukisha wapi,
Amepoteza mwelekeo anatafuta pa kutokea.
CCM sasa hivi Polisi ndio kimbilio lao,

Mwananchi akihoji kitu Jela,
Mwaandishi wa Habari akiandika kitu kuhusu Serikali Jela,
Vyama vya Siasa haviruhusiwi kufanya Siasa, Vikifanya Jela,
Na tena hii ni mbaya maana CCM wao kila siku wanafanya mikutano ya Kisiasa kupia Raisi, wakuu wa mikoa, Wakuu wa Wilaya, kiujumla CCM inafanya Siasa pekeyake kwa kutumia nguvu.

Ukiishiwa Sera ndio nguvu hutumika, CCM nguvu huwa zinazidiana kuweni makini.
 
Mambo hawayawezi wanayang'ang'ania wangemwachia Lowasee tu tucheke watz
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…