Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Lumumba watasema ww ni Ndulu unalalamika sbb umetumbuliwa...ila kila mmoja wao ipo siku watakuja kujua ukweli,wanao enjoy nchi hii ni Bashite na Kairuki tu
 
Mimi kila nikisikia anayofanya huyu jamaa,kwa kweli moyo unaniuma sana

Huyu anaharibu uchumi

Anaharibu demokrasia

Anaharibu kila kitu,huyu mtu ni kama kiwavi jeshi ndani ya shamba Tanzania

Nimekuelewa Kivuko Kibovu cha 1948=Tzs 8 Bil
 
Huna lolote...kama baba yako au wewe ulikuwa ni JIZI NA UTAWALA HUU UMEKUWA MUHANGA KWA HAYO MAOVU unashindwa nini kuandika hizi BHANGI HAPA.....
hata KIKWETE mlitukana hivi hivi......
Kwa hizi kelele zenu za kibangi bangi humu JF...zingekuwa zinareflect ukweli mbona WANANCHI wangeishakuwa wameingia BARABARANI.....
 
Rais anatupeleka kwenye uchumi wa kati, tanzañia ya viwanda na nchi ya wafanyakazi zinazotamvulika siyo wapiga dili.........kama unakaziyako unakuwaje na wasiwasi we jenga nyumba na peleka watoto shule wenzako ndo wanafanya hivyo ila kama ni mjanja mjanja mjini hapa tafuta kazi ulipe kodi....hayo tu.........sisi mbona rais tulishamuelewa kitaambo....
 
Ndugu wana JF,

Kwa moyo uliojaa simanzi napenda kuwauliza viongozi wetu wastaafu (Maraisi, Mawaziri, Wabunge, Makatibu), JE, MUSTAKABALI WA TAIFA LETU BADO UNAWAHUSU?

Ni kweli kwamba uongozi wa AWAMU YA 5 unajitahidi kufanya mengi mazuri na yanayostahili pongezi. Hata hivyo, naona MISINGI YA UTAWALA BORA NA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ni kama unatikisika. Swala la Uhuru wa kujieleza, vyama vya upinzani, uwajibikaji, Uhuru wa vyombo vya habari, nk imekua shida.

VIONGOZI WASTAAFU, Je, ni kweli hamna cha kumshauri kiongozi wetu kwa nia ya kuboresha utendaji wake? Tanzania bado inawahusu? Je, kazi yenu ni kusifia tu bila kuwa na ukosoaji (positive criticism).

* Mmelisikia swala la M-Nyet? Akiwa bado na tuhuma, kawa promoted.... Hii inavunja imani ya wananchi kwa vyombo vya usalama.

* Vyeti feki ni kwa baadhi ya watu, wengine hawagusiki.

Viongozi WASTAAFU, Je, TANZANIA BADO INAWAHUSU??

Mungu ibariki Tanzania.
 
Awamu ya pili ya ukombozi inalisubiri Taifa hili. Sio hawa viongozi.
 
Wanasikitisha na kustaajabisha sana kwa ukimya wao huku nchi ikizidi kwenda alijojo kwa jinsi huyu jamaa anavyopindisha sheria mbali mbali za nchi

Pia ukitilia maanani hivi karibuni aliwatusi kwamba wanawashwa washwa sidhani kuna atakayethubutu kutoa sauti yake.

 
Kila jambo likiguswa kwa ajili ya ukosoaji magufuli anajibu kwa kejeli na vijembe.
Nani yukotayari kujibiwa kwa vijembe utadhani Taarabu ya kike?

Mfano tu juzi kaambiwa kikwete kua anawashwa kweli atarudia kuongea chochote?
Mwana mipasho ndio wanamuogopa,visasi pia wanaogopa,

Maana unaweza ukunyang'anywa kilakitu chako alafu wanajificha kwenye kichaka cha uzalendo. Acha kabisa.
 
Kwa sasa tuna Taifa la hovyo sana unamfukuza muhongo na simbachawene kwa kashfa za matumizi mabovu ya ofisi za umma unamteua mnyeti kuwa mkuu wa mkoa kisa waliotoa habar wanatoka upande ambao hutaki kuusikia hili ni jambo la ajabu mno tena linalitia aibu taifa kiongozi ulieapa kuongoza kwa misingi ya sheria,haki na utu leo unageuza Taifa mali yako kauli na matendo yako ndo sheria sijui mnashangiliaga nini kuushinda upunzani ktk chaguzi mbalimbali ikiwa uwepo wao hautakiwi kwa mawazo ua hata kushiriki ktk nyanja mbalimbali za maendeleo ya Taifa hili kwa nini usifutwe kuokoa upotevu wa pesa zinazotolewa kama ruzuku?

Kuna vitu ukivifikiria kwa mapana na marefu vinaleta ukakasi mkubwa mno ndio mana kuna kiongozi mkubwa wa Taifa hili alihitaji sana kuombewa alishayajua matatizo yake huwezi ukiliongoza Taifa kwa kuligawa kwa itakadi za uvyama kiaisi hiki hili linaleta mahusiano mabovu miongoni mwa watanzania hizi nyufa zinazidi kutatuka kwa kasi kubwa mno kinachoongelewa na kiongozi wetu si matendo ayafanyayo amekuwa na mtu wa kuangalia ni nani wa kumshughulikia muda unavyozidi kwenda anazidi kupoteza imani na matumaini waliyokuwa nayo watanzania kwake.

Vitendo vya rushwa ni vigumu kufutika na vitaongezeka kwa kasi hasa kwa wale wanaovitumia kumfurahisha yeye.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…