Salamu wakuu, itifaki imezingatiwa
Hapo nyuma kidogo hii kazi ya teua tengua ilionekana kukoma na dalili za watu kufanya kazi zilianza kuonekana, majungu na unafiki ulikwisha kwa wale wategea teuzi za mkulu zaidi walijikita na kazi kwa nafasi walizonazo.
Hili zimwi limeibuka tena, juzi kati alichekecha baraza la mawaziri, akaamiza kichwa akapanga wakuu wa mikoa, hakusahau pia ile kazi ambayo huwa ni adhabu kwa wanatumbuliwa wakateuliwa pia(mabalozi)
Macho, masikio na matarajio ya waswahili wengi sasa tunasubiri teuzi za wakuu wa wilaya, huku nauhakika hutajaza nafasi zilizo wazi tu, natarajia watapunguzwa wengine na makada wengine wapewe nafasi.
Ni kazi nzito sana hii kwa Mh rais, majukumu haya yanakuumiza kichwa sana ni dhahiri utaishia teua tengua