Anayejua Rais Magufuli anatupeleka wapi atuambie, naona kama tumepotea

Status
Not open for further replies.
Sema ni mawazo yako,usitusingizie kuwa na sisi wananchi wa chini tunaona hivyo.Hayo ni mawazo yako binafsi na usituhusishe kwenye mawazo yako.Usibane au usitusemee.Pita hivi tuseme wenyewe.Natumbukia mimi
 
Rais Magufuli kesha tutoa huko, haturudi tena, SI LEO WALA KESHO. Hata Rais atakaye kuja baada ya Rais Magufuli hapo Novemba 2025 hatathubutu kuturudisha kwenye rushwa, wizi, utapeli, uncertainness ya kutokujua tunataka kwenda wapi. Rais Magufuli anajua na anataka tufike kwenye uchumi wa kati, uchumi wa viwanda na nchi yenye huduma za jamii za hali ya juu na za uhakika.
 
Dah dada angu umenimaliza kwa vicheko aisee.
Shukran umewaeleza hawa watu wa Nyerere Magu anajaribu kufanya nn.
kuna wengine wanajifanya hawaoni.
kuna sehemu nyingine kuna tatizo kubwa la maji hila JPM toka kaingia maji bwelele hadi raha alfu wanasema hawajui tunapopelekwa .

pyeeeeeee kubwa
 
Mbinu za kisasa za kujenga uchumi wa kati kwa kuhamasisha uwezekaji kwa wawekezaji wa nje na ndani na kuweka conducive and friendly investment scenarios ikiwa ni pamoja na good regulatory conditions to allow for a WIN WIN SITUATIONS.
Nilitaka kuona huo uchumi wa kati na maviwanda nabonyeza ngapi?

Niambie fasta nibonyeze chaaap
 
Kwanza hii miaka yake yote taifa limeipoteza bure ,Mnaomshabikia hebu tuambieni vizuri kwa uchambuzi yakinifu ,Jiwe wenu anasimamia nini ?kipaumbele chake nini?mipango yake iko category gani ? Muda mfupi ? Muda wa kati ?muda mrefu?Tuambieni mipango yake na Sera zake zinasaidiaje kuleta maendeleo ya kisiasa ,kijamii ,kiuchumi ,kiteknolojia na kisayansi ana mipango gani na amefanya nini mpaka sasa ?Mtujibu na mahusiano ya kimataifa na wawekezaji amefanya nini? na mipango yake ikoje kuvutia investors na kuleta mitaji na teknolojia mpya .
 
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam
Upanuzi wa barabara
Flyovers zinajengwa
Miradi ya umeme inajengwa na ni kwa hela za watanzania wenyewe
Utendaji kazi umeimarika,
Madawa sasa yanapatikana hospitali,
wafanyakazi wanawajibika
Hakika Namsifu Rais wetu.
 

We ni kula kulala Kwa Shemeji MTU aangaikae ndo uijua hali halisi
 
Chato.
 
Sawa kabisa wasiwasi nipale atakapo maliza muda wake mrithi wake atatumia formula inaitwaje mfano katika familia zetu kulikuwa na matajiri wenye pesa sana LUPONDUJE NA BANA BAKWE muda wao ulipo pita na mali zilipita nasisitiza Mfumo ni muhimu
 

Ni kwa kuwa huijui njia ndio maana unaona umepotezwa! Sisi tunaoijua njia yaani tunamuona kabisa amepiga 'diagonal' yaani short cut! Before you know it kana an yetu hiyo!
Just sit back & relax!
 
Nilitaka kuona huo uchumi wa kati na maviwanda nabonyeza ngapi?

Niambie fasta nibonyeze chaaap
Bonyeza website za ADB, IMF, CGTN, WORLD ECONOMIC LINK na nyingine za aina hiyo for indepth analysis na kukufungua na kukufumbua macho na kukuonyesha namna wendine wanavyo elezea safari ya Tanzania kwenye uchumi wa kati wa viwanda.
 
Mzee,najua kama unapita mitandaoni na kusoma maoni ya watu,basi unaweza kuona umefanikiwa sana kuwafanya watu wakuogope, ila jua tu unajidanganya kwani binadamu yoyote ana ukomo wa uvumilivu na wewe hutakuwa wa kwanza.

Elewa tu hata wasaidizi wako ambao sasa wanashambuliwa mitandaoni(wanaojaribu kukusitiri kwa gharama ya utu wao) watakuwa wanaumia na kujisikia vibaya na usishangae baadhi yao wakafikia ukomo na kuamua liwalo na liwe na wakawa wa kwanza kukuanika hata kwa kuwatumia watu wengine.

Hali inayoendelea sasa unatakiwa kuichukua kwa tahadhari na si kwa kuipuza hata kidogo.

Kumbuka,ukiharibikiwa,baadhi ya wanaokuzunguka na kukusifu ndio watakuwa wa kwanza kukukana na hata kukudhihaki.

Watu kama sisi kwa sasa tunaweza kuwa wa hovyo kwako, ila tambua kuna siku unaweza kuja kutuona tulikuwa wa maana kuliko waliochagua kukaa kimya na wale waliochagua kusifu kwa asilimia mia moja ingawa wanajua na wewe ni binadamu unaeweza/unaefanya makosa.

Badilika before it is too late.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…