Anayejua vyoo vya kuhamisha(mobile toilets) vinakokodishwa

Hahahaha unataka uwe unahama na nyaa zakoo
 
Kwa hapa Dar-es-slaam jaribu pale mahakama ya ndizi... Big brother upande wa kota za serikali naonaga kuna magari na vyoo vya kuhamisha huweka kwa ajili ya kukodishwa...

Angalizo usiende kwa Mariam Birian maanake yupo maeneo yale yale...


Cc: mahondaw
 
Ndugu zangu natafuta choo cha kukodi kinachohamishwa nisaidie mawasiliano niko Dar es salaam
Jaribu pale COTEX maenei ya Afrikana na Jogoo DSM. Kuna mfanyakazi aliwahi kunieleza mwaka jana kuwa wanayo na pia hutengeneza
 
Hebu mtafute yule rais kiduku Wa kule Korea ndo mtumiaji mzuri Wa hivyo vyoo akiwa safarini.....
 
Kuna yule kijana wa Mbeya aliunda helcopita ikakataliwa kuruka, ndiyo anatengeneza vyoo vya kuhama.
Namba zake sina ila uwasiliàne na sido Mbeya au makao makuu
 
Asante nashukuru
 
Nenda jirani kabisa na shule ya PERFECT VISION:vipo kama milioni moja hivi.
 
Ndugu zangu natafuta choo cha kukodi kinachohamishwa nisaidie mawasiliano niko Dar es salaam


Mkuu watafute CAPS Limited kupitia Mkurugenzi wao mmojawapo,wanafanya kazi ya kukodisha vyoo hivyo. Namba zao ni +255 713 606 644
 
Mkuuu hivyo vyoo kukodi bei iko juuu sana bei inaanzia 90,000 - 150,000/= kwa siku, kutegemea na Ubora wa Choo chenyewe. Pia bado usafirishajo wake ni delicate sana na gharama pia. Lkn kama huna haraka nacho ukienda SIDO wanavitengeneza kwa laki 9, hivyo kama unataka kwa matumizi ya Kiofissi ni heri mtengeneze kwa matumizi ya mara kwa mara.
Choo kipya kuagiza China manunuzi bei inaanzia 1.5 - 3.5 kulingana na ubora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…