Anayelifahamu ua hili zuri la manukato

Anayelifahamu ua hili zuri la manukato

Joined
Mar 12, 2021
Posts
9
Reaction score
15
Ua zuri lenye harufu ya kuvutia mi nalifahamu kwa jina la KILUA, haya maua nayaona sana maeneo ya pwani ebu wanayoyafahamu wanieleweshe zaidi kuhusu huu mti unaotoa haya maua.
20210312_085438.jpg
 
Mkilua ukifika jioni kunakua na harufu nzuri eneo lote ulipo huo mti kuna huu mkilua, mlangilangi, msomalia, asumini na waridi

Tunayatumia kama manukato unayachuma unayaweka kabatini harufu huenea au kama umekunja ngui zako unayaweka kati kati nguo zinatoa harufu nzuri, hii ni kwa kilua, mlangilangi, na msomalia

Muasumini na waridi maua yao hutumika pia kutengenezea kitu kinaitwa liwa, unayachukua maua yaliokauka unayaponda na kuyachekecha kwa kuyachanganya na karafuu, kisha unachukua unga uliopatikana unaweka katika jiwe unasugulia msio hapo ikisha unaviringisha kadonge tayari kutumika

Hutumika na wale wanawake wanaowekwa ndani tayari kusubiri kuolewa yani haina haja ya kuchubuliwa dada awe mweupe akisuguliwa mwilini na huo mchanganyiko mwili unakua mwororo

Maelezo ni marefu nimefupisha.
 
Yani kwa wewe Asante sana ila kama utapata nafasi ya kutuelimisha kwa mmea mmoja mmoja itakuwa na tija kwa jamii ya watu wanaopenda kuendezesha nyumba zao kwa maua
kwakweli me najua yanatumika kwa hivo labda kama kuna mwengine anajua aje aongeze elimu kwangu nimepanda muasumini na hua sisubiri yachanue kwenye mti wake hua nayachuma yakiwa hayachanua nayamwaga kitandani yanachanulia kitandani kunakua na natural scent flan hivi amazing chumbani
 
kwa wale wasiopenda harufu ya mafuta ya nazi hasa wale wanaopika wenyewe ukishapika tupia hayo maua yan yananukia vizur mno
 
kwakweli me najua yanatumika kwa hivo labda kama kuna mwengine anajua aje aongeze elimu kwangu nimepanda muasumini na hua sisubiri yachanue kwenye mti wake hua nayachuma yakiwa hayachanua nayamwaga kitandani yanachanulia kitandani kunakua na natural scent flan hivi amazing chumbani
Yaani nimekupenda bureeeeee asante sana
 
Zamani niliyatumia Sana kuyakunjia na nguo! Hasa milangilangi! Kueka juu ya kitanda kabla hujalala!, Pia unaweza ukayadunga na uzi ukafunga kichwani nywele zinanukia vizuri.
Kuna Yale mawardi(rose) unalieka kwenye glass ya maji unakunywa maji yenye harufu nzuri! Yana matumizi mengimengiiiii
 
Back
Top Bottom