Mkilua ukifika jioni kunakua na harufu nzuri eneo lote ulipo huo mti kuna huu mkilua, mlangilangi, msomalia, asumini na waridi
Tunayatumia kama manukato unayachuma unayaweka kabatini harufu huenea au kama umekunja ngui zako unayaweka kati kati nguo zinatoa harufu nzuri, hii ni kwa kilua, mlangilangi, na msomalia
Muasumini na waridi maua yao hutumika pia kutengenezea kitu kinaitwa liwa, unayachukua maua yaliokauka unayaponda na kuyachekecha kwa kuyachanganya na karafuu, kisha unachukua unga uliopatikana unaweka katika jiwe unasugulia msio hapo ikisha unaviringisha kadonge tayari kutumika
Hutumika na wale wanawake wanaowekwa ndani tayari kusubiri kuolewa yani haina haja ya kuchubuliwa dada awe mweupe akisuguliwa mwilini na huo mchanganyiko mwili unakua mwororo
Maelezo ni marefu nimefupisha.